NEW
Font size
WorksheetsAina za maneno
Total questions: 16
Worksheet time: 5mins
Sentensi gani kati ya hizi haina nomino?
Mama yangu ni mpishi hodari.
Alimpeleka hospitalini.
Mtumishi wa serikali amefika.
Lini Mwalimu atasahihisha mitihani?
Nomino ni nini?
Majina ya watu.
Majina ya watu, wanyama na vitu vyote.
Majina yanayotoa habari zaidi kuhusu wanyama.
Majibu yote si sahihi.
_________________ amefika shuleni. (Chagua jibu lisilo sahihi)
Mwewe
Mwalimu
Mbuzi
Kiti
Bawabu
___mekula chakula kilichobaki. (Chagua kiwakilishi mwafaka)
Zi
Ki
Wa
Ya
Yafuatayo ni aina ya maneno isipokuwa moja.
Vivumishi
Viwakilishi
Viundaji
Vitenzi
Nomino
Mto ni aina gani ya neno?
Nomino
Kitenzi
Kiwakilishi
Kielezi
Mama alimpata mtoto amelala kitandani. (aina gani ya neno lililopigiwa mstari?)
Kitenzi
Kielezi
Kivumishi
Nomino
Kielezi ni nini?
Jina la kitu, watu au mahali.
Neno linalotaja kitu.
Neno linalofafanua kitendo fulani.
Majibu yote ni sahihi.
Sentensi gani sio sahihi?
Aliyekuwa waziri wa Afya amefariki.
Amekuja nyumbani.
Amekuja mtoto nyumbani.
zote ni sahihi.
Mwanaharamia __________________ mashua. (Jaza nafasi kwa kitenzi sahihi.)
kilikamata
Yalikamata
Amekamata
walikamata
Alifungua lango asubuhi. (Neno gani limepigiwa mstari)
Kiwakiishi
Kielezi
Kivumishi
Kitenzi
Kivumishi ni nini?
Neno linalotoa habari zaidi kuhusu nomino
Neno lenye maana sawa na nomino.
Majina ya vitendo vya watu
Neno linalojisimamia.
Viwakilishi _______________________ nomino katika sentensi. (Jibu ipi sio sahihi?)
huwakilisha
haviwi pamoja na
vinakuwa pamoja na
vinasimama badala ya
__________ninapenda kuogelea.
Mimi
Yeye
Mtoto
Yule
Katibu yule ni mrefu. (chagua kivumishi)
Katibu
yule
ni
mrefu
Duma amemkimbiza na kumkamata Swara mbugani. (Chagua kielezi)
Swara
amemkimbiza
Duma
Mbugani.
