Wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

HHS Darasa la 5NORTH Kiswahili CAT

Total questions: 20

Worksheet time: 10mins

Name
Class
Date
1.

Mwanafunzi mgeni hutozwa _________ kama malipo ya kwanza anapojiunga na shule.

a)

koto

b)

karo

c)

fidia

d)

nauli

2.

Malipo ya kumshika mtoto kwa mara ya kwanza huitwa _________.

a)

ada

b)

fichuo

c)

fola

d)

kiokozi

3.

Tulilipa ______ tulipokuwa tukisafiri kwa matwana.

a)

sadaka

b)

kiingilio

c)

karo

d)

nauli

4.

Kisawe cha nomino ni _________.

a)

jina

b)

kitenzi

c)

kielezi

d)

ngeli

5.

Chakula cha mchana huitwa ______________.

a)

chajio

b)

chamcha

c)

staftahi

d)

kiamsha kinywa

6.

Kutokana na kitenzi lima tunapata nomino zifuatazo isipokuwa ____________.

a)

kilimo

b)

ukulima

c)

limiana

d)

mkulima

7.

Kutokana na kitenzi linda, tunaunda nomino ulinzi na pia _________.

a)

mlinzi

b)

lindwa

c)

askari

d)

lindana

8.

___________ ni shairi lenye mishororo minne kila ubeti.

a)

Takhmisa

b)

Tathlitha

c)

Tasdisa

d)

Tarbia

9.

Mtu anayetunga mashairi huitwa ________.

a)

Manju

b)

Malenga

c)

Sogora

d)

Mghani

10.

Mtu anayesafisha choo huitwa Chura au ___________.

a)

Msafishi

b)

Mwalimu

c)

Mwimbaji

d)

Topasi

11.

_____________ ni vazi la ndani la kuficha uchi.

a)

Kanchiri

b)

Kamisi

c)

Kocho

d)

Kanzu

12.

Kaptura pia huitwa ____________.

a)

gagro

b)

surupwenye

c)

bombo

d)

chupi

13.

Kanusha: Amekula chakula. ___________________.

a)

Hajala chakula.

b)

Hatakula chakula.

c)

Hali chakula.

d)

Hakuli chakula.

14.

Andika kwa wingi: Ukuta huu ni mrefu. _____________________.

a)

Ukuta hizi ni refu.

b)

Kuta hizi ni ndefu.

c)

Nyuta hizi ni refu.

d)

Makuta haya ni marefu.

15.

Nomino kitabu linapatikana katika ngeli ya ____________.

a)

Ki-Vi

b)

Li-Ya

c)

I-Zi

d)

A-Wa

16.

Nomino kipofu linapatikana katika ngeli ya ____________.

a)

Ki-Vi

b)

Li-Ya

c)

I-Zi

d)

A-Wa

17.

Upinde wa mvua una rangi ____________.

a)

sita

b)

saba

c)

tano

d)

nne

18.

Kifungu kimoja katika shairi huitwa ____________.

a)

mshororo

b)

ubeti

c)

kibwagizo

d)

kina

19.

Kitambaa ambacho hutundikwa kwenye dirisha huitwa _____________.

a)

pazia

b)

zulia

c)

mto

d)

mkeka

20.

Koti fupi lisilo na mikono huitwa _________.

a)

sketi

b)

kizibao

c)

ovaroli

d)

fulana