wayground logo

Free Printable Worksheets

NEW

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI

Total questions: 12

Worksheet time: 6mins

Name
Class
Date
1.

Ni kipi miongoni mwa vifuatavyo kisichotumika jikoni?

a)

Chano

b)

Fyekeo

c)

Buli

d)

Bilauri

2.

Jua huchomoza upande wa __________.

a)

Magharibi

b)

Kaskazini

c)

Kusini

d)

Mashariki

3.

Daftari la kuandikia lina umbo gani?

a)

Mche

b)

Kopa

c)

Mstatili

d)

Mraba

4.

Mtoto wa mjukuu wangu nitamwitaje?

a)

Mpwa

b)

kitukuu

c)

Kilembwe

d)

Kinying'inya

5.

Mnyama wa msituni anayefanana na nguruwe ni ________

a)

nyati

b)

kifaru

c)

ngiri

d)

swara

6.

Anayemsaidia daktari hospitalini kwa kuwapa wagonjwa dawa na kuhakikisha wamekula anaitwa _____________.

a)

tabibu

b)

mchuuzi

c)

msusi

d)

mwuguzi

7.

Ni nini hutumika pamoja na kinu kutwangia vitu jikoni?

a)

Mche

b)

Mbuzi

c)

Mchi

d)

Buli

8.

Ni vazi lipi huvaliwa na wanawake pekee?

a)

Kanchiri

b)

Suruali

c)

Koti

d)

Kizibao

9.

Rangi ya juu ya upinde wa mvua ni __________ .

a)

machungwa

b)

samawati

c)

nyekundu

d)

kijani

10.

Yupi kati ya wanyama wafuatao ni tofauti na wengine?

a)

Sokwe

b)

Kima

c)

Swara

d)

Tumbiri

11.

Samaki ni kwa maji kama vile ndege ni kwa ___________ .

a)

kombe

b)

kizimba

c)

mzinga

d)

kiota

12.
  1. Kati ya shughuli hizi, ni ipi huja ya kwanza?
a)

Kupanda

b)

Kulima

c)

Kupalilia

d)

Kuvuna