wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

Kiswahili

Total questions: 15

Worksheet time: 5mins

Name
Class
Date
1.

Kamilisha kwa amba-: Rinda _______ anavaa ni safi

a)

ambao

b)

ambayo

c)

ambalo

d)

ambacho

2.

Jina gani liko katika ngeli ya U-I

a)

mtume

b)

maji

c)

mwewe

d)

mwembe

3.

Kamilisha methali: Asiyekujua _________

a)

hakujui

b)

hakuthamini

c)

hakuamini

d)

hakujali

4.

Tegua kitendawili: Halima wangu mwembamba ni fundi wa kuungaunga ______

a)

Ufagio

b)

sindano

c)

kiberiti

d)

sungura

5.

Neno lipi si la adabu?

a)

Nataka

b)

Mjamazito

c)

Kundradhi

d)

Samahani

6.

Nini wingi wa: Bata mdogo anaogelea kwenye bwawa.

a)

Bata wadogo wanaogelea kwenye bwawa.

b)

Mabata wadogo wanaogelea kwenye bwawa.

c)

Bata wadogo wanaogelea kwenye mabwawa.

d)

Mabata wadogo wanaogelea kwenye mabwawa.

7.

Tumia -ngine: Nyumba _____ zitajengwa

a)

nyingine

b)

ingine

c)

mingine

d)

mengine

8.

Upi si msamiati wa sebuleni?

a)

takia

b)

shubaka

c)

chano

d)

rafu

9.

Kamilisha methali: Mwenda tezi na omo _________

a)

hana ajualo

b)

marejeo ngamani

c)

huwa mwema

d)

atakuunguza

10.

Mjomba au shangazi yako anakuita ________ wake

a)

umbu

b)

mpwa

c)

mkoi

d)

binamu

11.

Unapoenda kwenye msiba wa kifo, utawaambia waliofiliwa, "Makiwa!" nao watakujibu

a)

Tunayo

b)

Sawa

c)

Asante

d)

Poa

12.

Mtu anayefanya kazi ya kujenga kwa matofali au mawe huita ___________

a)

mjenzi

b)

mwashi

c)

msukaji

d)

mwezekaji

13.

Tumia -enye: Mwembe _____ maembe mabivu ni ule.

a)

yenye

b)

lenye

c)

wenye

d)

chenye

14.

Lipi si jina lililoko katika ngeli ya I-ZI?

a)

sakafu

b)

samani

c)

sahani

d)

shavu

15.

Mfalme huishi kwenye kasri, naye rais huishi kwenye ___________

a)

ikulu

b)

bunge

c)

makavazi

d)

mahakama