NEW
Font size
WorksheetsWANYAMA WA MAJINI
Total questions: 21
Worksheet time: 7mins
Samaki mkubwa kuliko samaki wote bararini,mwenye ngozi ngumu ya kijivu, meno makubwa makali anayekula watu.
PAPA
NYANGUMI
NGUVA
PWEZA
Mnyama mkubwa wa bahari mwenye umbo kama la samaki, mwenye mafuta mengi na hunyonyesha kama wanyama wengi.
TAA
NYANGUMI
DAGAA
KIBOKO
Samaki wa rangi ya fedha wenye umbo dogo sana ambao hawawezi kukua zaidi.
PAPA
MKUNGA
SANGARA
DAGAA
Kidudu kinachoishi ndani ya kombe.
PWEZA
KOCHE
CHAZA
SANGARA
kiumbe wa baharini mwenye gamba gumu jeusi, mwili mrefu uliogawanyika sehemu sehemu, miguu minane na mikono miwili yenye makucha ya kushikia ambaye anapopikwa gamba lake hubadilika na kuwa jekundu.
KOCHE
CHURA
KIBOKO
CHAZA
samaki mkubwa wa baharini mwenye umbo bapa na mkia mwembamba mrefu.
MKUNGA
DAGAA
KAMBA
TAA
samaki mwenbamba mrefu mwenye umbo la nyoka ambaye ni mweusi au wa kijivu, kahawia ay mabatobato.
PAPA
NGUVA
MKUNGA
MAMBA
samaki wa maji baridi mwenye kichwa kikubwakigumu cha bapa na masharubu marefu.
KONOKONO
CHURA
TAA
KAMBARE
Mnyama wa baharini mwenye mikia minane.
PWEZA
NGUVA
KIBOKO
KAMBA
Mnyama wa jamii ya kenge lakini mkubwa zaidi ambaye ana magamba na huishi kwenye maji.
POMBOO
MAMBA
KIBOKO
NYANGUMI
Mnyama mkubwa anayeishi mitoni au katika maziwa na mabwawa mwenye masikio madogo, meno makubwa na mapana na pua pana yenye mianzi mipana.
KIBOBO
NYANGUMI
PAPA
MAMBA
Mnyama mdogo wa baharini mwenye magamba laini na miguu mingi ambayr huliwa.
KAMBA
TAA
MAMBA
DAGAA
Samaki mkubwa mrefu mwenye kivimbe cha duara na rangi ya kijivu aishiye baharini.
KAMBA
KAMBARE
NGURU
PWEZA
Samaki wa maji baridi, wa jamii ya perege aliye na umbo kubwa na mdomo mpana.
MKUNGA
KONOKONO
PAPA
SANGARA
Mnyama mdogo wa majini mwenye miguu sita au Zaidi na gamba mwilini.
KOCHE
PAPA
PWEZA
KAA
Mnyama wa baharini anayenyonyesha watoto wake mwenya umbo la binadamu
MAMBA
NGUVA
KIBOKO
NYANGUMI
Mnyama wa baharini afananaye kobe.
TAA
KASA
DAGAA
PAPA
Samaki mkubwa wa baharini anayefanana na papa
PWEZA
KIBOKO
POMBOO
NGURU
Mnyama mwenye ngozi laini asiye na mkia
SANGARA
CHAZA
SAMAKI
CHURA
Mnyama mdogo anayeteleza na kutambaa polepole
CHURA
KAMBA
KONOKONO
PWEZA
Kiumbe anayeishi majini mwenye mapezi-fins na mkia
MAMBA
TAA
CHURA
SAMAKI
