NEW
Font size
WorksheetsKISWAHILI SHAIRI
Total questions: 40
Worksheet time: 40mins
Shairi lililo na vipande vitatu huitwaje?
Utenzi
Ukwapi
Ukawafi
Mathnawi
Ukawafi
Gani kati ya hizi bahari siyo inayotokana na idadi ya vipande?
Ukawafi
Mathnawi
Ukara
Utendi
Shairi lililo na neno maalum katika kila ubeti huitwaje?
Kikai
Mandhuma
Kikwamba
Sabilia
Shairi lililo na kipande kimoja kifupi kuliko kingine huitwaje?
Kikai
Ukara
Ukaraguni
Msuko
Shairi lililo na mshororo mmoja mfupi kuliko mingine huitwaje?
Kikai
Mandhuma
Utenzi
Msuko
Ikiwa hoja kwenye shairi linakamilishwa kwenye kipande kinachofuata katika kila mshororo, shairi hilo hujulikanaje?
Mathnawi
Upindu
Kikwamba
Mandhuma
Ni neno gani lisilo na maana sawa kwa shairi linaloanzishwa na maneno yanayolimaliza?
Upindu
Mkufu
Nyoka
Sabilia
Shairi lililo na bahari zaidi ya moja hujulikana vipi?
Sabilia
Mtiririko
Sakarani
Kikwamba
Shairi lisilo na kibwagizo huitwaje?
Sakarani
Sabilia
Msuko
Mandhuma
Shairi lenye vipande viwili kwa kila mshororo hujulikana vipi?
Mathnawi
Mazda
Ukawafi
Ukara
Shairi lenye urari wa vina huitwaje?
Masivina
Shairi huru
Mtiririko
Ukaraguni
Shairi lisilo na urari wa vina huitwaje?
Shari huru
Kikai
Masivina
Tumbuizo
Shairi lenye kipande kimoja kwa kila mshororo huitwa?
Masivina
Mathnawi
Ukawafi
Utenzi
Shairi lililo na vina vinavyobadilika kutegemea ubeti huitwaje?
Ukaraguni
Ukara
Mtiririko
Sabilia
Shairi ambalo vina vya kipande kimoja hubadilika na vya kipande kingine kubakia vile vile huitwaje?
Ukaraguni
Ukara
Ukwapi
Mathnawi
Shairi lililo na vina vinavyobadilika kutegemea ubeti huitwaje?
Ukaraguni
Ukara
Mtiririko
Sabilia
Gani kati ya hizi siyo idhini ya kishairi?
Tabdila
Mazida
Inkisari
Tarbia
Mshororo wa tatu wa shairi huitwaje?
Mloto
Ukwapi
Mleo
Utao
Shairi lenye vipande vinne huitwaje?
Mavue
Mleo
Ukawafi
Mathnawi
Kipande cha tatu kwenye shairi huitwaje?
Mwandamo
Mavue
Ulingo
Ukwapi
Shairi lisilo na urari wa vina wala mizani ni?
Mavue
Masivina
Shairi huru
Shairi guni
Shairi lenye mizani minane kwa kila kipande ni?
Ukawafi
Tumbuizo
Ukingo
Tathlitha
Kwa kueleza umbo la shairi, kigezo hiki hakizingatiwi. Kipi?
Idadi ya mishororo
Idadi ya vipande
Idadi ya mizani
Kurudiwa kwa kibwagizo
Kutumia misamiati ya jadi ni uhuru gani kwenye shairi?
Lahaja
Utohozi
Tabdila
Ukale
Kufupisha maneno kwenye shairi kwa kutumia king'ong'o ni idhini gani?
Inkisari
Mazda
Lahaja
Ritifaa
Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti huitwaje?
Mavue
Tathlitha
Tarbia
Mathnawi
Shairi ambalo neno la mwisho huanza ubeti unaofuata huitwaje?
Upindu
Nyoka
Zingo
Mkufu
Neno nyuta liko katika ngeli gani?
I-ZI
U-ZI
U-YA
I-I
Neno kitungule linapatikana kwa ngeli gani?
KI-VI
I-ZI
A-WA
I-I
Taja ngeli ya uhubiri
U-YA
U-U
I-ZI
U-ZI
Umoja wa mitume ni?
Mitume
Tume
Mtume
Utume
Gani kati ya hizi siyo sifa bainifu ya sauti /b/?
Kipasuo
Hutamkwa mdomoni
Hafifu
Ghuna
Mbinu ya kifasihi ambayo huhusisha upigaji wa picha akilini huitwaje?
Taharuki
Latifa
Taswira
Takriri
Methali ifuatayo ina mbinu gani ya kifasihi?
Tamaa mbele mauti nyuma.
Taashira
Tanakuzi
Jazanda
Balagha
Wewe ni wembe ni mbinu gani?
Tashhisi
Tashbihi
Istiara
Jazanda
Bainisha mbinu katika kitendawili hiki. Huku ng'o na kule ng'o
Kitendawili
Tanakali ya sauti
Takriri
Tashtiti
Hadithi ambapo mhusika hukabiliwa hali ngumu ya kuamua baina ya mambo mawili au zaidi yanayomkabili huitwaje?
Ngano za mazimwi
Ngano za mtanziko
Mighani
Visasili
Ngano ya majitu huitwaje?
Ngano za mazimwi
Ngano za mtanziko
Mighani
Soga
Andika sentensi hii kwa wingi:
Dereva alipomwona askari, alishusha abiria haraka.
Dereva alipowaona maaskari, aliwashusha maabiria haraka.
Madereva walipowaona askari, waliwashusha abiria haraka.
Madereva walipowaona askari, waliwashusha maabiria haraka.
Dereva alipowaona maaskari, aliwashusha abiria haraka.
Neno gani halipatikani katika ngeli ya LI -YA?
Jembe
Limau
Karatasi
Tunda
