WorksheetsKISWAHILI
Total questions: 15
Worksheet time: 5mins
Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?
(i) shtaka (ii) somea (iii) sinia (iv) sebule
iv, i, iii, ii
iv, ii, i, iii
iv, iii, i, ii
iv, i, iii, ii
Ni jibu lipi lenye mpangilio sahihi wa aina za maneno katika sentensi ifuatayo?
Wanafunzi hawa ni hodari kuliko wengine.
nomino, kivumishi, kitenzi, kivumishi, kihusishi, kiwakilishi;
nomino, kitenzi, kiwakilishi, kivumishi, kihusishi, kivumishi;
nomino, kielesi, kitenzi, kivumishi, kiunganishi kiwakilishi;
nomino, kielezi, kitenzi, kihusishi, kiunganishi, kivumishi.
Ni jibu lipi lisiloambatanishwa ipasavyo?
koo jimbi
mjomba halati
shaibu buda
mavyaa bavyaa
Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi.
ita — mwito
sahau — sahaulifu
agiza — maagizo
vumilia — uvumilivu
Ni sentensi ipi inayoonyesha kusudi la tendo?
Suna aliingia zizini akawafungulia ng’ombe, akaelekea malishoni.
Malika alituambia twende tukavue samaki.
Wafanyakazi walifanya bidii wakamaliza kazi hiyo.
Wageni watakuja watakapokamilisha shughuli.
Sentensi, ‘Sauna aliwafanya Siki na Patu waandike insha,’ inamaanisha;
Sauna aliwaandikisha Siki na Patu insha.
Sauna aliwaandikishia Siki na Patu insha.
Siki na Patu walimwandikia Sauna insha.
Siki na Patu waliandikia insha kwa Sauna.
22. Chagua jibu lenye viambishi vya neno: funguliana.
fu-a-na
. li-an-a
fu-an-a
li-a-na
Chagua senstensi iliyoafikishwa ipasavyo.
Vifaa vyote — vile vilivyoagizwa jana — vimeletwa.
Lo, hilo kubwa hivyo, utaliweza?
Magunia haya hayatoshi! tutanunua mengine.
Mweka hazina (aliyeteuliwa) hapa jana rit (mwenye) bidii.
Ni sentensi ipi iliyo katika hali timilifu?
Magari hayapiti hapa siku hizi.
Mitaro hiyo haijachimbwa vyema.
Nguo yake haikuoshwa ipasavyo.
Wimbo hautaimbishwa na kiongozi.
Onyesha sentensi iliyounganisha sentensi zlfuatazo ipasavyo.
Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo.
Makaa hakufaulu.
Mithili ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.
Licha ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.
Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo madhali hakufaulu.
Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo walau hakufaulu.
Chagua sentensi yenye kivumishi kiulizi.
Leo wameapishwa wangapi?
Wasusi, wanaelekea wapi?
Huyu atavikwa pete gani?
Mashubaka haya yalitengenezwa lini?
Chagua usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo.
“Shule zitafunguliwa lini?” Yohana akauliza.
Yohana alitaka kujua wakati ambapo shule zingefunguliwa.
Yohana aliuliza ikiwa shule zitafunguliwa.
Yohana aliuliza wakati ambapo shule zinafunguliwa.
. Yohana alitaka kujua ikiwa shule zingefunguliwa.
Methali “Fimbo ya mbali haiui nyoka” huambiwa mtu anayetegemea walio mbali kutatulia matatizo yake. “Kiserema hulima kikashinda jembe zima,” huambiwa:
Mtu anayejiona kuwa maarufu sana katika jambo kuliko wengine.
Mtu anayedhauliwa na wengine japo ana uwezo mkubwa
Mtu anayedharau matatizo yake kuliko ya wengine.
Mtu anayepuuza makubaliano ya wengine kuliko yao.
Ikiwa juzi ilikuwa Jumanne, mtondo itakuwa:
Ijumaa
Jumapili
Jumamosi
Jumatatu
Akisami, 3/8 kwa maneno ni:
sudusi tatu
thuluthi nane
tusui nane
thumni tatu
