WorksheetsKISWAHILI 005 2021
Total questions: 16
Worksheet time: 5mins
Kukanusha kwa: ‘Mtumbwi ambao ulinunuliwa
umeanza safari‘, ni:
Mtumbwi ambao ulinunuliwa haukuanza safari.
Mtumbwi ambao haukununuliwa haujaanza safari.
Mtumbwi ambao ulinunuliwa haujaanza safari.
Mtumbwi ambao haukununuliwa haukuanza safari.
Chagua usemi halisi wa sentensi ifuatayo:
Mwenesi alimwambia ndugu yake kuwa wangeenda Mombasa siku ambayo ingefuata.
“Kesho mtaenda Mombasa.“ Mwenesi
alimwambia ndugu yake.
“Siku iliyofuata mlienda Mombasa.” Mwenesi alimwambia ndugu yake.
“Kesho utaenda Mombasa.” Mwenesi alimwambia ndugu yake.
“Siku iliyofuata ulienda Mombasa.” Mwenesi alimwambia ndugu yake
Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Mruka kiunzi alipongezwa aliponyakua nishani hiyo.
Waruka viunzi walipongezwa waliponyakua nishani hiyo.
Waruka viunzi walipongezwa waliponyakua nishani hizo.
Mruka viunzi alipongezwa aliponyakua nishani hiyo.
Mruka viunzi alipongezwa aliponyakua nishani hizo.
Ikiwa mtondogoo itakuwa Jumanne, leo ni:
Jumamosi
Alhamisi
Ijumaa
Jumatano.
Chagua sentensi yenye kiwakilishi kimilikishi.
Mzazi wake alihudhuria sherehe Iakini wangu hakuhudhuria.
Mtoto wao aliamka mapema lakini huyu alichelewa.
Mfanyakazi wa tatu alistaafu lakini wengine walibakia.
Msafiri wa nne alipata kibali lakini waie hawakupata.
Natu ameolewa na John. Dada yake Natu ameolewa na Ken. Ken na John wataitana:
mwamu
mwanyumba
kivyere
mkwe.
Ni kundi lipi lenye viunganishi pekee?
maadamu, kama, kefule, hamadi
ijapokuwa, ila. wala, bali
labda, ingawa, ikiwa, hata
sembuse, tangu, badala, basi.
Shehena ni ya mizigo ilhali ni _____ la udongo.
tita
peto
shumbi
bumba.
Chagua sentensi yenye maelezo sahihi.
Hijabu ni ugonjwa wa kuvimba fizi.
Kimeta ni ugonjwa unaodhofisha figo.
Tauni ni ugonjwa unaokatakata viungo.
Surua ni ugonjwa wa kutoa vipele.
Ni sentensi ipi yenye matumizi sahihi ya koloni?
Jumapili ni tarehe: 3.3.2012.
Mama alinunua matunda: yaani, chungwa, fenesi na embe.
Teknolojia imefanikisha maendeleo: akasema waziri.
Miji niliyotembelea ni hii: Kisumu, Nairobi, Voi na Embu.
Gugu ni nyasi ndefu zinazomea katika sehemu tambarare, gugu pia ni
mmea unaotambaa kote shambani;
mmea unaobana mingine shambani;
mmea unaomea pale pasipopaliliwa;
mmea unaomea mahali usipotakikana.
Chagua jibu lenye maelezo sahihi.
Mjumu ni fundi wa kufua visu.
Sogora ni bingwa wa kuimba mashairi ngomani.
Dalali hushindania bidhaa mnadani.
Mkalimani hutafsiri maandishi vitabuni.
Sentensi, ‘Jedi ni ninga’ imetumia tamathali gani?
Msemo
Tashbihi
Sitiari
Nahau.
Arbuni ni __________________
sehemu ya bei ya kitu inayotolewa mwanzoni;
sehemu ya ujira wa kumsaidia mtu mwanzoni;
sehemu ya fidia anayolipwa mtu mwanzoni;
sehemu ya malipo ya kukopea kitu mwanzoni.
Methali, ‘Kamba ya mbali haifungi kuni’, ni kwa wanaotegemea msaada wa walio mbali.
‘Maji ya kifuu bahari ya chungu’. ni kwa:
anayeiona hadhi ya vitu kuwa ya chini;
anayeyaona matatizo ya wengine kuwa madogo;
anayeziona hali za wengine kuwa za kawaida.
anayeviona vitu vidogo kuwa na faida chache.
Methali, ‘Kamba ya mbali haifungi kuni’, ni kwa wanaotegemea msaada wa walio mbali.
‘Maji ya kifuu bahari ya chungu’. ni kwa:
anayeiona hadhi ya vitu kuwa ya chini;
anayeyaona matatizo ya wengine kuwa madogo;
anayeziona hali za wengine kuwa za kawaida.
anayeviona vitu vidogo kuwa na faida chache.
