WorksheetsMAHAKAMANI
Total questions: 10
Worksheet time: 10mins
Mahakama ni jengo ambalo hutumiwa kwa shughuli za kusikiliza na kuamua kesi. Je, mwanasheria ambaye husikiliza na kukata kesi huitwa nani?
Wakili
hakimu
Kiongozi wa mashtaka
Karani wa korti
Mtu anapokamatwa na polisi, hufungwa nini mikononi ili asitoroke?
vikuku
pingo
vipingu
nyororo
Katoti alipatikana na hatia ya wizi wa ng'ombe baada ya jaji kuamua kesi yake. Je, Katoti alilipa malipo yapi kati ya haya?
Dhamana
Fola
Fidia
Faini
Wakati wa kusikiliza kesi kuhusu wizi wa kimabavu, shahidi mmoja alitoa video aliyorekodi wizi huo ulipofanyika. Video hii ni mojawapo ya ushahidi ambao huitwa______
idhibati
ithibati
dungu
ushuhuda
Mfanyakazi wa mahakamani ambaye huwasaidia washtakiwa, washtaki au mashahidi kula yamini anaitwa___
Karani wa korti
Kiongozi wa mashtaka
Wakili
mahabusu
Ni nini maana ya kuruka kesi?
Kukubali kesi ili ikamilike haraka
Kukataa kukubali kesi ili ushahidi utolewe.
Kushinda kesi
Kukwepa kesi kwa ujanja
Kwa kawaida kortini huwa na vizimba vingapi?
A. mbili
B. viwili
C. moja
D. kimoja
Ni nani kati ya hawa hastahili kuwa na wakili?
mshtakiwa
Mshtaki
Shahidi
Kiongozi wa mashtaka
Eleza maana ya semi 'kutiwa mbaroni'
Kufikishwa mahakamani kwa sababu ya kudaiwa kutenda uovu
Kuvungwa pingu baada ya kukamatwa na polisi
hali ya kukamatwa na polisi kwa sababu ya kushukiwa kuvunja sheria
Kufungiwa katika rumande ili kesi isikilizwe siku nyingine.
_______________ ni mtu ambaye alikamatwa na polisi na amefikishwa mahakamani akasomewa mashtaka yake.
wakili
mshtakiwa
mshukiwa
mfungwa
