NEW
Font size
WorksheetsSarufi:Aina za Maneno
Total questions: 25
Worksheet time: 53mins
Panga maneno haya kama yanavyopatikana katika kamusi
i.Chimba
ii.Chimbua
iii.Chimbo
iv.Chimbia
i,ii,iii,iv
iv,i,iii,ii
i,iv,iii,i
iii,ii,i,iv
Sahihisha sentensi ifuatayo:
Darasani waliopo wanafunzi mna jasho nyingi
Darasa waliopo wanafunzi pana jasho nyingi.
Darasani waliomo wanafunzi mna jasho nyingi.
Darasani waliomo wanafunzi mna jasho jingi.
Darasa walipo wanafunnzi mna jasho mingi
Kunitania anakonitania kunaniudhi sana.Ngeli iliyotumika ni gani?
Ki-Vi
Pa-Ku-Mu
Ku-Ku
I-Zi
Ni sentensi gani sahihi?
Pazia zote zimeanikwa nyasini.
Vyura vyote vilikufa maji yalipokauka.
Mapua ya ng'ombe hayaliki.
Majiko yamewashwa na wajakazi.
Tumia viambishingeli vifaavyo kujaza pengo;
Ndizi hi__ __bivu ni __dogo sana
o;m;n
zi;m;n
li;m;n
le;m;n
Maneno yafuatayo yanapatikana katika ngeli gani?
Uwele,Utete,Ulezi
U-U
U-Ya
U-Zi
U-I
Ngeli ya A-Wa hujumuisha viumbe wenye uhai,nayo ya Pa-Ku-Mu ni ya
Vitenzi
Nomino
Mahali
Wingi
Ni nomino gani ambayo ni ya dhahania?
Maziwa
jozi
mwizi
urembo
Ni kundi lipi lenye nomino za kawaida pekee?
Mlolongo,umati,genge
Mwalimu,mnyama,chakula
mti,Nairobi,Mbwa
Pakashume,Mwekahazina,mwananchi
Kiwakilishi ni neno ambalo husimamia____________
kitenzi
kivumishi
kielezi
nomino
Mpira huu na ule yote ni ya kandanda.
Maneno yaliyopigwa kijistari yametumikaje?
Kimilikishi,kisifa
kivumishi,kiwakilishi
kielezi,kiwakilishi
kisifa,kielezi
Tambua kihusishi:
Wamesimama kando ya barabara wakisubiri gari.
wakisubiri
gari
wamesimama
kando ya
Jaza kwa kihusishi kifaacho zaidi
Ndege wengi hujenga viota_________________mti.
chini ya
juu ya
miongoni mwa
kando ya
Mbona unatembea bila sweta_______________kuna baridi.
ilhali
iwapo
sembuse
na
"Ki" imetumikaje katika sentensi ifuatayo?
Kiendacho kwa mganga hakirudi.
kielezi
masharti
wakati
kiwakilishi
Nitawaona watakapokuja kesho
Viwakilishi vilivyopigwa mstari ni vya
nafsi ya kwanza na ya tatu
nafsi ya pili na ya kwanza
nafsi ya kwanza na ya pili
nafsi ya pili n aya tatu
Tambua kiwakilishi katika sentensi hii
Wengine badoo wanaendeleza ukabila.
bado
wengine
ukabila
wanaendeleza
Mkifika msikitini mtapata babu akiali.
Neno lililopigwa mstari ni ?
kielezi cha namna
Kielezi cha mahali
Kielezi cha idadi
kielezi cha wakati
Mwali amekula maembe mengi sana
Neno lililopigwa mstari ni________________
kielezi
kivumishi
kibadala
kiwakilishi
Kutokana na kitenzi "ogopa" tunapata nomino "mwoga".Kutokana na kitenzi "iba" tunapata nomino___________
mwiba
mwizi
mwibaji
mwibi
Tuliandikiana barua naye.
Kauli gani imetumika?________________________
kutendana
kutendeana
kutenda
kutendeeana
Vitenzi pia huitwa___________________?
nomino
vibadala
visifa
viarifa
Nyambua katika kauli ya kutendesha:
oa;jua;kaa
olesha;juza;ketisha
olesha;juvya;kasha
oza;juvya;kalisha
oza;julisha;kasha
Tumia kiunganishi kifaacho kujazia pengo.
Mwana wa mnyama hufuata amri___________________wa binadamu.
isipo
ila
kaifa
mintarafu
Nitupie mpira huo.
Maana ya sentensi hii ni__________________
Utupe mbali,utupe kwa niaba yangu.
Utupe nilipo,utupe mbali
Utupe kwako,utupe mahali fulani
Utupe kwa niaba yangu,utupe nilipo
