WorksheetsReview Intro Kiswahili II
Total questions: 17
Worksheet time: 54mins
Wewe ukoje? (umri na sifa) (Describe yourself in a full sentence, including your age and at least 3 descriptive ajectives)
Maggie ni mtoto wa ngapi? (Jibu kwa sentensi nzima)
(a)
Hiki ni kitanda cha rangi gani? (Answer with "hiki ni (a) ")
Leo umevaa mavazi gani?
Hawa wamevaa nguo gani?
Kanga hii ina rangi gani?
Jina la kanga hii lina maana gani kwa Kiingereza? (Mungu = God)
Kanga hii ina rangi gani?
Jina la kanga hii lina maana gani kwa Kiingereza? (Kuogopa = to be afraid of)
Hii ni nini?
Bajaji
Meli
Teksi
Pikipiki
Hiki ni chombo gani cha kusafiri?
Basi
Teksi
Bodaboda
Daladala
Wewe husafiri vipi kwenda kazini au chuoni?
What are two different ways to ask a guest what kind of drink he/she would like?
Ungekuwa na uwezo, ungesafiri wapi? (jibu kwa sentensi nzima)
Kwa: Hubert.Smith@gmail.com
Kutoka: Salima.Hassan@gmail.com
tarehe: 12.08.22
yahusu: Karibu Dar es Salaam
Mpendwa Hubert,
Nimefurahi sana kusikia utakuja kututembelea hapa Dar es Salaam. Karibu sana!
Mimi na watoto wangu wawili, Juma na Neema, tutakuja kukupokea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam siku hiyo utakapokuja. Utanijua kwa sababu mimi ni mrefu sana na nitavaa mtandio mwekundu kichwani. Pia nitavaa gauni la kitenge la rangi mbalimbali -- rangi nyekundu, rangi ya manjano, na ranji nyeusi. Juma ni mtoto mdogo -- ana miaka minne tu. Yeye atavaa kaptula ya rangi ya buluu na tisheti nyeupe. Neema ana miaka kumi na mmoja. Yeye atavaa gauni la rangi ya zambarau na rangi ya waridi na viatu vya rangi ya waridi. Anapenda sana rangi ya waridi! Yeye pia ni mcheshi -- ninafikiri utapenda kuzungumza naye.
Kesho yake, tutembee ufukweni (ufukwe=beach) na familia nzima. Nimeambatisha picha ya ufukwe ulioko karibu na nyumbani kwetu. Je, unapenda kuogelea? Usisahau kuja na nguo za kuogelea baharani. Lakini ukisahau, tunaweza kwenda sokoni kununua nguo mpya.
Wewe utavaa mavazi ya rangi gani siku ya safari?
Je, utakuja na rafiki yako au utakuja peke yako tu?
Wako,
Mama Neema
Hubert anasafiri wapi?
Hubert anasafiri Nairobi
Hubert anasafiri Dar es Salaam
Hubert anasafiri Zanzibar
Hubert hasafiri
Hubert atamjuaje Mama Neema?
Mama Neema ni mrefu
Mama Neema atavaa suruali ya buluu
Mama Neema anapenda rangi ya waridi
Mama Neema atavaa mtandio mwekundu
Neema anapendelea rangi gani?
Rangi ya Zambarau
rangi ya buluu
rangi ya manjano
rangi ya waridi
Siku ya kumpokea Hubert uwanja wa ndege, Mama Neema atavaa mavazi gani?
Juma ana miaka mingapi?
(a)
Kwa nini Mama Neema anafikiri kwamba Hubert atapenda kuzungumza na Neema?
Mama Neema anataka Hubert aende wapi na familia? Anamwambia asisahau nini?
Write the question "Have you (s.) slept well?" and the answer "No, I have not slept well." in Kiswahili.
(a)
What are two different ways to ask for the price of something in Kiswahili?
