wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI

Total questions: 20

Worksheet time: 20mins

Name
Class
Date
1.

Picha hii ina mmea mchanga. Je, mmea mchanga huitwaje?

a)

mchi

b)

mche

c)

mimea

d)

mparachichi

2.

Andika sentensi ifuatayo kwa umoja?

Mihogo yao imeiva.

a)

mhogo wake umeiva

b)

muhogo wake umeiva

c)

muhogo wao umeiva

d)

muhogo wangu umeiva

3.

Mmea unaozaa kahawa huitwa_______

a)

mche

b)

kahawa

c)

mbuni

d)

mgomba

4.

Ndizi huwa na utamu mwingi. Je, mmea unaozaa ndizi huitwaje?

a)

mndizi

b)

mpera

c)

mpunga

d)

mgomba

5.

Mmea huu huzaa maembe. Wingi wake ni miembe. Umoja wa miembe ni __________

a)

embe

b)

myembe

c)

mwembe

d)

muhogo

6.

Mmea huu huitwa mpunga. Je, unazaa zao gani?

a)

wali

b)

mchele

c)

parachichi

d)

mahindi

7.

Mtu anayeimba mashairi huitwa_____

a)

mshororo

b)

manju

c)

malenga

d)

mghani

8.

Kipofu, mtume, chura, kipepeo na bata ni nomino zinazopatikana katika ngeli ya ________

a)

KI-VI

b)

A-WA

c)

LI-YA

d)

U-I

9.

Nomino darasa, magari, goti, tumbo, daftari na madawati hupatikana katika ngeli gani?

a)

LI-YA

b)

KI-VI

c)

A-WA

d)

U-I

10.

Mshororo unaorudiwarudiwa katika shairi huitwaje?

a)

malenga

b)

kibwagizo

c)

shairi

d)

tarbia

11.

________ni shairi la mishororo minne katika kila ubeti.

a)

tathmina

b)

tarbia

c)

tathlitha

d)

tathnia

12.

Chombo kinachotumiwa kuonyesha pande za dunia huitwa__________

a)

jua

b)

dira

c)

kochi

d)

jokofu

13.

Jua huchomoza kutoka upande wa ___________

a)

kaskazini

b)

kusini

c)

magharibi

d)

mashariki

14.

Bendera ya nchi yetu ina rangi nne. Je, ni rangi gani husimamia ardhi?

a)

nyeusi

b)

nyekundu

c)

kijani kibichi

d)

nyeupe

15.

Maneno yafuatayo huitwaje?

papa-baba

pipi-bibi

koti -goti

a)

kinyume

b)

vitate

c)

visawe

d)

kielezi

16.

Neno lililopigiwa mstari ni mfano wa neno gani ya Kiswahili?

Mayai matano yamevunjika.

a)

kielezi

b)

kivumishi

c)

nomino

d)

kitenzi

17.

Hii ni suruali ya miguu mifupi ambayo hujulikana kama kaptura au _____

a)

kocho

b)

bombo

c)

kamisi

d)

sare

18.

Mavazi haya huvaliwa na wachezaji. Je , yanaitwaje?

a)

sare

b)

jezi

c)

chupi

d)

daluga

19.

Maneno yafuatayo huitwaje?

Ebo!, Lo!, Masalaale!, Aha!, Kumbe!, Huree!, Alhamdulillahi!, Hoyee!

a)

viwakilishi

b)

vihusishi

c)

vihisishi

d)

vielezi

20.

Jaza pengo kwa kutumia kiunganishi kifaacho.

Hakunywa chai _______uji.

a)

lakini

b)

wala

c)

na

d)

pia