wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

2 Timotheo Quiz

Total questions: 25

Worksheet time: 15mins

Name
Class
Date
1.

Nani aliyeandika kitabu cha 2 Timotheo?

a)

Yohana

b)

Paulo

c)

Petro

d)

Luka

2.

Ni nini mada kuu ya 2 Timotheo?

a)

Uvumilivu, ukarimu na wema

b)

Hekima, maarifa, na ufahamu

c)

Uvumilivu, uaminifu, na ustahimilivu

d)

Upendo, Furaha na amani

3.

Je, kuna sura ngapi Katika 2 Timotheo?

a)

3

b)

6

c)

5

d)

4

4.

Ni nini umuhimu wa maneno 'Maana Mungu alitupa sisi roho si ya woga, bali ya nguvu na upendo na kiasi' Katika 2 Timotheo?

a)

Kishazi hiki kinamaanisha kwamba waumini wanapaswa kuzingatia tu hofu na kupuuza uwezo, upendo, na kujitawala.

b)

Inapendekeza kwamba waumini wanapaswa kutanguliza woga badala ya nguvu, upendo, na kujitawala.

c)

Kishazi hicho kinasisitiza haja ya waumini kuishi kwa hofu na kuepuka nguvu, upendo, na kujitawala.

d)

Kishazi hicho kinasisitiza haja ya waumini kuishi pasipo hofu na kuzinatia nguvu, upendo, na kiasi .


5.

Timotheo alikuwa nani kwa mtume Paulo?

a)

kaka.

b)

Mshirika wa karibu na mfanyakazi mwenza

c)

mwalimu

d)

jirani

6.

Ni nini kusudi la Paulo kuandika waraka wa 2 Timotheo?

a)

Kumtia moyo, kumkumbusha na kumfundisha Timotheo


b)

Kumkatisha tamaa, kusahau, na kutomjali Timotheo


c)

Kuchanganya, kupotosha, na kumdanganya Timotheo


7.

Je, ni baadhi ya mistari gani muhimu katika 2 Timotheo ambayo inasisitiza uvumilivu katika Imani?


a)

2 Timotheo 4:7-8, 2 Timotheo 2:3-4


b)

2 Timotheo 4:3-4


c)

2 Timotheo 1:1-2

d)

2 Timotheo 3:5-6

8.

Ni maagizo gani ambayo Paulo alimpa Timotheo kuhusu kushughulikia mafundisho ya uwongo katika 2 Timotheo?

a)

Epuka kusahihisha mafundisho ya uwongo ili kudumisha amani

b)

Lihubiri neno; kuwa tayari wakati wa msimu na nje ya msimu; sahihisha, kemea na kutia moyo—kwa saburi kubwa na mafundisho makini.

c)

Kupuuza mafundisho ya uongo na kuzingatia ukuaji wa kibinafsi

d)

Pambana na mafundisho ya uwongo kwa ukali bila subira

9.

2 Timotheo inawahimizaje waumini katika kuvumilia mateso?

a)

Kwa kuwalaumu waumini kwa mateso na ukosefu wao wa imani

b)

Kwa kupendekeza waumini kuacha imani yao ili kuepuka mateso

c)

Kwa kuwakumbusha waamini thawabu ya milele na kukazia umuhimu wa kuendelea kuwa waaminifu kwa Mungu licha ya magumu.

d)

Kwa kupuuza mateso na kujifanya kila kitu kiko sawa

10.

Je, ni wosia gani wa mwisho aliopewa Timotheo na Paulo?

a)

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake hudumu milele.

b)

Lihubiri neno; uwe tayari wakati ukufaao na wakati usiokufaa; karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. - 2 Timotheo 4:2

c)

Mwimbieni Bwana wimbo mpya; nchi na imwimbie Bwana.

d)

Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

11.

Paulo alimwonya Timotheo kuhusu nyakati za hatari katika nyakati za (a)   .

12.

Kupenda pesa ndio mzizi wa (a)   yote.

13.

Paulo alimtia moyo Timotheo kupigana vile vita vizuri, kumaliza shindano la mbio, na kushika (a)   .

14.

Paulo katika 2 Timotheo 2:2 anamsihi Timotheo kufanya nini na mafundisho aliyoyapata kwake?

a)

kuyashika na kuyafundisha kwa watu wote.

b)

kuonya,kufundisha kwa uvumilivu wote.

c)

kuwakabidhi watu waaminifu watakao fundisha wengine.

d)

kuilinda Imani tuliyopewa mara moja tu.

15.

ushiriki taabu yangu kama...............................mwema wa Kristo. imenakiliwa katika sura ya pili.

a)

mtumishi

b)

Askari

c)

kiongozi

d)

mwanafunzi

16.

lakini msingi wa Mungu ulio Imara umesimama , wenye muhuri hii......................................................

a)

Bwana Yesu anarudi

b)

Mungu ni mwaminifu

c)

Bwana awajua walio wake na tena kila alitajae jina la Bwana na aache uovu.

17.

Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Kutokana na mistari hiyo , Ni chombo gani cha kupata heshima ?

a)

Mtu ampendaye Bwana kwa moyo wote,akili zote na mali zake zote.

b)

mtu mtakatifu amgonjea Bwana kwa Saburi.

c)

mtu aliyejitakasa na kujitenga na waovu.

d)

aliyemwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

18.

Maswali ya upumbavu yasiyo ya elimu yakataliwe. maswali haya yana athari ipi?

a)

huzaa magomvi

b)

huharibu wasikiao

c)

huleta ubishi

d)

huathiri utakatifu.

19.

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu (a)  

Ni adha gani inayowapata watu wanaotaka kuishi maisha ya utauwa.

20.

Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa...................

a)

wana masikio ya utafiti

b)

hawamjui Mungu

c)

hawaijui kweli ya Mungu

21.

kwa muktadha wa sura ya nne , mtume paulo alikuwa Katika wakati gani ?

a)

wakati wa kifungo.

b)

wakati wa safari yake ya umisheni.

c)

wakati wa utumishi

d)

wakati wa kufariki

22.

Mtume paulo anathibitisha kuwa taji hatopewa mwenyewe bali na.........................................

(kama ilivyo Katika sura ya nne)

a)

watu wote wamngojea Bwana.

b)

watu wote wampendao Bwana.

c)

watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

d)

watu wote walioshiriki mateso Pamoja nae.

23.

mwisho wa waraka huu, mtume paulo anamtahadharisha Timotheo juu ya Iskanda mfua shaba akimsihi ajiepushe nae. ni sababu ipi anaitoa?

a)

alihubiri injili nyingine tofouti na injili yetu.

b)

aliyapinga sana maneno yetu.

c)

hakuyakubali maneno ya uzima.

d)

aliniacha na kufuata ulimwengu.

24.

Paulo mtume anaomba nini juu ya wote waliomwacha Katika jawabu lake la kwanza?

a)

Mungu awalipe kwa kadri ya matendo yao.

b)

Mungu awasamehe.

c)

neema na rehema za Mungu ziwe juu yao.

d)

wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.

25.

Katika sura ya pilli , Paulo amemfananisha Timotheo kama askari, mwanamichezo na (a)  

Akionesha jinsi mtenda kazi anabidi awe na juhudi na uvumilivu.