Font size
WorksheetsKISWAHILI JARIBIO LA PILI
Total questions: 20
Worksheet time: 59mins
Nomino ni mojawapo ya vipengele katika lugha ya Kiswahili.
Je, ni kundi lipi la nomino ambalo pia huitwa nomino mahususi?
Vitenzijina.
Nomino za pekee.
Nomino fungamano.
Nomino dhahania.
Chagua nomino ya pekee kutoka kwa sentensi hii.
Mwalimu alipoingia darasani, Jembe alimuuliza ruhusa ya kuenda msalani.
Jembe.
Mwalimu.
Ruhusa.
Msalani.
Chagua kitenzijina ambacho hakijaandikwa vyema.
Kula.
Kulala.
Kucheza.
Kukufa.
Nomino za vitu ambavyo haviwezi kuhesabika na hupatikana tu katika wingi kama vile: maji, marashi na maziwa huitwa nomino za wingi au nomino (a)
Ni sentensi ipi iliyoandikwa katika wakati uliopo hali endelezi?
Mvua ya kidindia ilikuwa ikinyesha hapa kwetu.
Mvua ya kidindia itakuwa ikinyesha hapa kwetu
Mvua ya kidindia ingali inanyesha hapa kwetu.
Mvua ya kidindia hunyesha hapa kwetu kila siku.
Badilisha sentensi hii iwe katika wakati ujao hali timilifu.
Shule yetu imefungwa mapema sana.
Shule yetu itakuwa imefungwa mapema sana.
Shule yetu imekuwa imefungwa mapema sana.
Shule yetu itakuwa ikifungwa mapema sana.
Shule yetu ilikuwa imefungwa mapema sana.
Sentensi zifuatazo hazijaandikwa sahihi ila moja tu.
Ni gani sahihi?
Baba wa Musa angekuwa na pesa, angalimnunulia Musa gari.
Wanafunzi wote walikuwa wanasoma kwa bidii.
Kesho, wanafunzi watakuwa wanafanya zoezi.
Mimi ningekuwa na uwezo, ningewasaidia watu maskini.
Andika kitenzi lala katika kauli ya kutendeshwa.
laliswa
lazwa
lalizwa
lashwa
Badilisha sentensi hii iwe katika kauli ya kutendwa.
Mkulima alipanda mimea mingi .
Mkulima alipandisha mimea mingi.
Mkulima alipandiwa mimea mingi.
Mimea mingi ilipandiwa kwa mkulima.
Mimea mingi ilipandwa na mkulima.
Andika kitenzi CHEKA katika kauli ya kutendea
(a)
Kuna tanzu mbili za fasihi.
Fasihi andishi na Fasihi_____________
simulia
simulisi
simulizi
tamthilia
Mtu ambaye huwasilisha fasihi simulizi kama vile hadithi huitwa (a)
Ni maelezo yapi hapa yanahusu tamthilia?
Huwa na wahusika wachache.
Mandhari yake ni finyu
Hurudiwarudiwa.
Huwa na maneno elekezi katika mabano.
Chagua maelezo yasiyohusu tamthilia.
Tamthilia hupangwa katika maonyesho.
Huwa na muundo wa dayolojia.
Huweza kuigizwa kwenye jukwaa.
Huwa fupi kuliko novela.
Soma kisa hiki kisha uyajibu maswali yanayofuata.
Mandhari ya kisa hiki ni wapi?
Nyumbani.
Sokoni.
Shuleni.
Kanisani.
Taja maudhui yanayojitokeza katika kisa hiki.
Usafi wa mazingira.
Ajali za sokoni.
Huduma ya kwanza.
Kuanguka sokoni.
Kwa nini mama wa Diba alianguka chini?
Mama wa Diba alianguka chini kwa sababu alikuwa na haraka.
Mama wa Diba alianguka chini kwa sababu alisukumwa na watu sokoni.
Mama wa Diba alianguka chini kwa sababu alikanyaga maganda ya ndizi.
Mama wa Diba aliangusha na kishindo kikuu.
Andika ukubwa wa nomino kiti.
Jiti
Jikiti
Jijikiti
Kijikiti
Andika udogo wa nomino kitu.
(a)
Andika wingi wa ukubwa wa:
Mwanamke mrefu alimchinja ng'ombe mkubwa.
Wanawake warefu waliwachinja ng'ombe wakubwa.
Majanajike marefu yaliwachinja magombe makubwa.
Majanajike marefu yalichinja magombe makubwa.
Majanajike marefu yaliyachinja magombe makubwa.
