wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI QUIZ

Total questions: 17

Worksheet time: 13mins

Name
Class
Date
1.

Ni _____ uumie kwa sasa ili upite mtihani wako.

a)

kabisa

b)

mradi

c)

tafadhali

d)

bora

2.

Chagua Kivumishi cha idadi katika sentensi ifuatayo.

Watoto wanne watakao pita mtihani watapata zawadi maalum.

a)

wanne

b)

watakao

c)

maalum

d)

watoto

3.

Ni sentensi ipi iliyoandikwa kwa wakati uliopita?

a)

Gari limepata ajali sasa

b)

Mjomba aliniahidi zawadi

c)

Mama amepika chakula kitamu

d)

Safari itakuwa ya kesho.

4.

Andika udogo wa sentensi ifuata

Ng'ombe wao si mkubwa

a)

Ng'ombe chao si kikubwa

b)

Kigombe chao si kikubwa

c)

Gombe lao si kubwa

d)

King'ombe chao si mkubwa

5.

Taja salamu za jioni au usiku katika orodha ifwatayo _____

a)

sabalkheri

b)

buriani

c)

chewa

d)

masalkheri

6.

Ni magari ____ yana abiria?

a)

yupi

b)

zipi

c)

vipi

d)

yapi

7.

Mmea unaotupatia mchele huitwaje?

a)

Mkanju

b)

Mbuni

c)

Mgomba

d)

Mpunga

8.

Ugali _____ ulikuwa mtamu sana.

a)

wenye

b)

ile

c)

hiyo

d)

wenyewe

9.

Andika kwa wingi

Mtu anayesoma hupita vizuri.

a)

Watu wanawosoma hupita vizuri.

b)

Watu anayesoma hapiti vizuri.

c)

Vijitu vinavyosoma hupita vizuri.

d)

Watu wanaosoma hupita vizuri.

10.

Kanusha sentensi ifuatayo.
Wageni wanatutembelea kwetu.

a)

Wageni hawajatutembelea kwetu

b)

Wageni hawatutembelei kwetu

c)

Wageni hawakututembea kwetu

d)

Wageni hawatatutembelea kwetu

11.

Istiara 'Kamene ni kinyonga' ina maana gani?

a)

Ni kigeugeu

b)

Ana rangi nyingi

c)

Ana maringo

d)

Anajipenda sana

12.

Babake ni mkono birika. Hii sentensi inamaanisha kuwa babake ni

a)

mgonjwa

b)

mto

c)

mkarimu

d)

mchoyo

13.

Tumia amba:
Chakula alichokila kilikuwa na sumu.

a)

Chakula ambacho alikila kilikuwa na sumu

b)

Chakula alichokila ambacho kilikuwa na sumu

c)

Chakula ambacho alichokila kilikuwa na sumu

d)

Chakula ambacho alikikula kilikuwa na sumu

14.

Kinyume cha mjomba ni _____.

a)

mjukuu

b)

mkoi

c)

shangazi

d)

halati

15.

Mtu napomkosea mwenzake huomba msamaha kwa kusema?

a)

makiwa

b)

pole

c)

simile

d)

niwie radhi

16.

Barau nyingi kwa pamoja ni _.

a)

bahasha

b)

kikosi

c)

kigaro

d)

kipeto

17-20.

Soma kifungu kisha ujibu maswali

Kila Jumamosi, Mama yetu huenda sokoni na kutuachia shughuli za kutekeleza nyumbani. Mimi ndimi Mwanambee. Mama huniambia niwe mwangalizi akiwa na shughuli za nje. Kaka zangu wawili na dada zangu watatu hunisaidia kufanya shughuli za ndani. Ni watiifu. Daima hawakaidi maagizo yangu. Jumamosi moja, mama aliondoka kwenda sokoni kama alivyozoea. Tuliamua kuzigawa kazi ili tumalize kabla hajarejea. Niliwaambia dada zangu wafue, wasafishe nyumba na kutayarisha chamcha. Kaka zangu walipaswa kufyeka nyasi ndefu na kuulenga ua. Ghalla, nilimsikia mbuzi wetu akilia lo! Ni nani atakayewashughulikia wanyama hawa? Nikauliza.

17.

Je, familia ya kina mwandishi ina jumla ya watu wangapi?

(a)  

18.

Kulingana na ufahamu, ni kweli kusema kuwa watoto katika familia hii

a)

hufanya shughuli zao kwa ushirikiano

b)

kila mara hufanya shughuli zao kwa haraka

c)

wamejawa na kiburi na majivuno

d)

ni wazembe kupindukia

19.

Mwishowe, ni nani ambaye aliwashughulikia wanyama wa kina mwandishi?

a)

Mwandishi mwenyewe

b)

Kaka wa mwandishi

c)

Baba wa mwandishi

d)

hatujaambiwa

20.

Kwanini mwandishi na ndugu zake waligawa kazi?

(a)