Wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

GREDI YA SABA 001

Total questions: 10

Worksheet time: 34mins

Name
Class
Date
1.

Nomino ni neno ambalo hutaja kiumbe, mahali au hali. Chagua nomino ambayo inataja mahali.

a)

chakula

b)

huzuni

c)

Nairobi

d)

maji

2.

Kuna aina tofauti za nomino. Ni aina gani za nomino ambazo pia huitwa nomino fungamano?

a)

Nomino za wingi

b)

Nomino dhahania

c)

Vitenzi-jina

d)

Nomino za kawaida

3.

Chagua nomino ya pekee katika orodha hii...

a)

leo

b)

dawati

c)

unywele

d)

Jumamosi

4.

Soma sentensi hii kwa makini..

Mwanafunzi mwerevu alienda Marekani.

Je, ni gani nomino ya kawaida katika sentensi hii?

(a)  

5.

Herufi kubwa hutumiwa katika njia hizi zote isipokuwa.....

a)

Mwanzoni mwa sentensi

b)

Kuandika mada au kichwa

c)

kuandika tarehe

d)

mwanzoni mwa nomino mahususi/pekee

6.

Tazama na utambue matumizi ya herufi kubwa katika sentensi hii.

Wanafunzi wanafurahia mtaala wa elimu wa C.B.E.

a)

Mwanzoni mwa sentensi na kufupisha maneno.

b)

Mwanzoni mwa nomino ya pekee na kufupisha maneno.

c)

Mwishoni mwa sentensi na kufupisha maneno.

d)

Kuandika mada na kufupisha maneno.

7.

Chagua sentensi ambayo imetumia kivumishi cha sifa.

a)

Mtoto huyu anajua kupika chai.

b)

Askari wawili waliwalinda watoto.

c)

Nyumba ndefu ni ya kina Maria.

d)

Shule ya kwanza kufunguliwa ilikuwa ya Bidii.

8.

Hizi zote ni nomino fungamano. Gani si nomino fungaano?

a)

nywele

b)

maji

c)

maziwa

d)

marashi

9.

Je, barua ya kirafiki huwa na anwani ngapi?

a)

tatu

b)

mbili

c)

moja

d)

haina hata moja

10.

Wanafunzi wanne walifanya mambo tofauti. Ni yupi ambaye alizingatia usafi wa kibinafsi?

a)

Suzana: Aliwalisha kuku wa mama yake.

b)

Maina: Alisafisha darasa lake na kupanga madawati.

c)

Kibet: Alipiga mswaki na akapiga miguu yake sulu.

d)

Dorina: Alipanda maua na kufyeka nyasi ndefu karibu na nyumba yao.