NEW
Font size
WorksheetsSarufi na matumizi ya lugha
Total questions: 41
Worksheet time: 21mins
Kanusha. Tumewasalimu wote kwa pamoja
Hatujamsalimu wote kwa pamoja
Hatukuwasalimu wote kwa pamoja
Tujawasalimu wote kwa pamoja
Hatujawasalimu wote kwa pamoja
Ukikanusha kwa wings sentensi hii, jibu litakuwa? Ukishiba niambie
Usiposhiba usiniambie
usiposhiba niambie
ukishiba usiniambie
Ukiwa haujashiba usiniambie
Nyambua katika hali ya kutendesha. La-
Lalisha
Laza
Lisha
Liza
Nyambua katika hali ya kutendewa. Fa-
Fawa
Fiwa
Faliwa
Filiwa
Nyambua katika hali ya kutendea. Nya-
Nywea
Nyolea
Nyoea
Nyea
Ni jibu gani linaloeleza vizuri zaidi maana ya fasihi simulizi?
Fasihi inayosemwa watu wanapokaa.
Fasihi inayohusu masimulizi kama vile ya riwaya.
Fasihi inayowasilishwa kwa mazungumzo na kuhifadhiwa akilini.
Fasihi inayohifadhiwa akilini ingawa wakati mwingine huwa vitabuni.
Ni sifa zipi zinazotambulisha fasihi kama sanaa?
Lugha yenye ufundi/ina umbo maalum/husawiri mandhari/hujenga wahusika kwa ustadi.
Ina masimulizi/ina umbo maalum/ina matukio/hujenga wahusika kistadi.
Lugha yenye ufundi/ina maelezo/ina umbo maalum/ husawiri mandhari.
Ni ipi si dhima ya fasihi simulizi katika jamii?
Kuliwaza.
Msingi wa kuunganisha watu.
Kuimarisha uzalendo.
Kitambulisho cha kundi fulani.
Kutatua migogoro ya kijamii.
Kamilisha: Fasihi simulizi huwa na hadhira hai ilhali fasihi andishi______________.
ina hadhira yenye mchanganyiko.
ina hadhira isiyoonekana ana kwa ana na mwandishi.
ina hadhira inayoweza kujitokeza na kutoweka.
ina hadhira inayosoma na kusikiliza.
Tambua sentensi inayosema ukweli kuhusu fasihi simulizi.
Fasihi simulizi ni mali ya serikali ilhali fasihi andishi ni mali ya kibinafsi.
Fasihi simulizi ina hadhira pana kuliko fasihi andishi.
Fasihi simulizi ina tanzu chache kuliko za fasihi andishi.
Fasihi simulizi ina historia fupi kuliko fasihi andishi.
Ni zipi tanzu za fasihi simulizi?
Ngano/ Semi/ Mazungumzo/ Maigizo/ Ushairi Simulizi.
Hadithi/ Misemo/ Mazungumzo/ Maigizo/ Ushairi Simulizi.
Hadithi/ Semi/ Mazungumzo/ Maigizo/ Ushairi Simulizi.
Hadithi/ Semi/ Mazungumzo/Uigizaji/ Ushairi Simulizi.
Ni vipi fasihi simulizi imeathiri fasihi andishi kimaudhui/dhamira?
Maswala mengi katika fasihi andishi ndiyo yamejadiliwa katika fasihi simulizi.
Lugha inyotumiwa katika fasihi simulizi ndiyo hutumiwa kwenye fasihi andishi.
Wahusika wa fasihi simulizi ndio hujitokeza katika fasihi andishi.
Utendaji wa fasihi simulizi unaweza kujitokeza katika fasihi andishi, thibitisha.
Kuna uigizaji jukwaani wa fasihi andishi kama vile tamthilia.
Fanani anaweza kuimba anapotembea.
Msomaji wa riwaya anaweza kuimba/kucheza anaposoma.
Ni mambo gani yanayochangia kubadlika kwa fasihi simulizi?
Hadhira/ Muktadha wa wakati/ Fanani.
Hadhira/ Ploti/ Muktadha wa wakati.
Hadhira/ Wahusika/ Fanani.
Ni ipi siyo sifa ya fasihi simulizi?
Ina utendaji.
Ni hai.
Ina mahali teule pa uwasilishaji.
Historia yake ni fupi.
Ina wakati maalum wa kuwasilishwa.
Ni kipera kipi kisichohusiana na vingine?
Riwaya.
Tamthilia.
Hadithi.
Novela.
Ni kipera kipi kisichohusiana na vingine?
Riwaya.
Tamthilia.
Hadithi.
Novela.
Kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi, ni gani hubadilika kwa urahisi?
Fasihi simulizi.
Fasihi andishi.
Zote hubadilika kwa urahisi.
Zote hazibadiliki kwa urahisi.
Tambua kauli ambayo ni kweli.
Fasihi simulizi huhitaji maandalizi kabla ya kutolewa.
Fasihi simulizi haihitaji maandalizi kabla ya kutolewa.
Fasihi andishi haihitaji maandalizi kabla ya kuandika.
Fasihi andishi huhitaji mazungumzo kabla ya kuandika.
Fanani ni nani?
Mtu anayesikiliza uwasilishaji wa kazi ya fasihi simulizi.
Mtu anayeeleza mafunzo yanayotokana na kazi ya fasihi simulizi.
Mtu anayetunga na kuwasilisha kazi ya fasihi simulizi.
Msanii anayefurahia kazi ya fasihi simulizi.
Ni ipi si kipera cha hadithi?
Vitendawili
Visasili
Mighani
Visakale
Nini maana ya fani?
Mbinu zinazotumiwa na fanani kuwasilisha maudhui.
Mbinu zinazotumiwa na hadhira kutambua wahusika.
Mbinu zinazotumiwa na fanani kuwasilisha nyimbo.
Mbinu zinazotumiwa fanani kutenda kazi za fasihi simulizi.
Tambua kundi lenye vipengele vya fani.
Ploti/ Wahusika/ Nyimbo.
Ploti/Vitabu/ Nyimbo.
Ploti/Wahusika/Hadithi.
Mhusika ni nini?
Viumbe wanaotajwa na fanani anapowasilisha wimbo.
Viumbe wa kweli wanaotumiwa kuwasilisha ujumbe katika kazi ya fasihi.
Viumbe wa kisanaa wanaotumiwa kuwasilisha ujumbe katika kazi ya fasihi.
Malighafi kuu ya fasihi kama sanaa ni_______________.
Hadithi
Lugha
Msanii
Kalamu
Sentensi gani kati ya hizi haina nomino?
Mama yangu ni mpishi hodari.
Alimpeleka hospitalini.
Mtumishi wa serikali amefika.
Lini Mwalimu atasahihisha mitihani?
Nomino ni nini?
Majina ya watu.
Majina ya watu, wanyama na vitu vyote.
Majina yanayotoa habari zaidi kuhusu wanyama.
Majibu yote si sahihi.
_________________ amefika shuleni. (Chagua jibu lisilo sahihi)
Mwewe
Mwalimu
Mbuzi
Kiti
Bawabu
___mekula chakula kilichobaki. (Chagua kiwakilishi mwafaka)
Zi
Ki
Wa
Ya
Yafuatayo ni aina ya maneno isipokuwa moja.
Vivumishi
Viwakilishi
Viundaji
Vitenzi
Nomino
Mto ni aina gani ya neno?
Nomino
Kitenzi
Kiwakilishi
Kielezi
Mama alimpata mtoto amelala kitandani. (aina gani ya neno lililopigiwa mstari?)
Kitenzi
Kielezi
Kivumishi
Nomino
Kielezi ni nini?
Jina la kitu, watu au mahali.
Neno linalotaja kitu.
Neno linalofafanua kitendo fulani.
Majibu yote ni sahihi.
Sentensi gani sio sahihi?
Aliyekuwa waziri wa Afya amefariki.
Amekuja nyumbani.
Amekuja mtoto nyumbani.
zote ni sahihi.
Mwanaharamia __________________ mashua. (Jaza nafasi kwa kitenzi sahihi.)
kilikamata
Yalikamata
Amekamata
walikamata
Alifungua lango asubuhi. (Neno gani limepigiwa mstari)
Kiwakiishi
Kielezi
Kivumishi
Kitenzi
Kivumishi ni nini?
Neno linalotoa habari zaidi kuhusu nomino
Neno lenye maana sawa na nomino.
Majina ya vitendo vya watu
Neno linalojisimamia.
Viwakilishi _______________________ nomino katika sentensi. (Jibu ipi sio sahihi?)
huwakilisha
haviwi pamoja na
vinakuwa pamoja na
vinasimama badala ya
__________ninapenda kuogelea.
Mimi
Yeye
Mtoto
Yule
Katibu yule ni mrefu. (chagua kivumishi)
Katibu
yule
ni
mrefu
Duma amemkimbiza na kumkamata Swara mbugani. (Chagua kielezi)
Swara
amemkimbiza
Duma
Mbugani.
