Wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

DARASA LA NANE

Total questions: 15

Worksheet time: 8mins

Name
Class
Date
1.

Mhudumu wa ofisini anayetumwa kupeleka barua na habari ni ____________

a)

mshenga

b)

tarishi

c)

mtumwa

d)

mhazili

2.

Anayetafsiri lugha moja hadi nyingine ni _______________

a)

mjumbe

b)

haini

c)

mhafidhina

d)

mkalimani

3.

Anayefundisha mwari kunga za nyumbani huitwa somo au ___________

a)

kungwi

b)

mganga

c)

mjumu

d)

mlowezi

4.

Anayefanya kazi ya kubeba mizigo kwa mkokoteni ni ______

a)

wakala

b)

beba

c)

hamali

d)

topasi

5.

Anayewasuka wanawake nywele huitwa msusi au _________

a)

msonzi

b)

mtunzi

c)

msasi

d)

kinyozi

6.

Anayeuza maji kwa kuyatembeza ni ___________

a)

kuli

b)

mzegazega

c)

mrumba

d)

nokoa

7.

Mtu anayeosha,kufagia na kusafisha vyoo ni ______________

a)

topasi

b)

mwosha

c)

mfagizi

d)

mpambe

8.

Achungaye wanyama wanaopandwa kama vile farasi ________

a)

msasi

b)

msana

c)

saisi

d)

sarahangi

9.

Stadi wa kucheza ngoma ni ____________

a)

katikiro

b)

mutribu

c)

manju

d)

sogora

10.

Mtu mwenye tabia ya kueneza habari za uongo ni _______

a)

sakubimbi

b)

shushushu

c)

karagosi

d)

mwandazi

11.

Anayepakia na kupakua mizigo kwenye meli ____________

a)

kuli

b)

lugojo

c)

mamluki

d)

mpagazi

12.

Anayewakilisha nchi yake katika nchi nyingine ni ___________

a)

jasusi

b)

mhaini

c)

diwani

d)

balozi

13.

Anayeweka hesabu ya pesa ni _______________

a)

mhazili

b)

mhasibu

c)

mlariba

d)

mhandisi

14.

Anayetabiri mambo kwa kutumia elimu ya nyota ni ___________

a)

mramali

b)

mrasimu

c)

mratibu

d)

msajili

15.

Anayewaita Waislamu msikitini kwenda kuswali ___________

a)

mhariri

b)

kadhi

c)

mwadhini

d)

imamu