NEW
Font size
WorksheetsZOEZI
Total questions: 20
Worksheet time: 15mins
Jaza pengo kwa usahihi.
Gari ______limenunuliwa na mwanaspoti aliyepewa tuzo.
nzuri
zuri
mazuri
mzuri
Tegua kitendawili kifuatacho.
Kuku wangu anatagia mibani.
yai
uyoga
mwavuli
nanasi
Ni saa ngapi?
saa tatu na robo
saa tatu kasorobo
saa tatu kamili
saa tisa kasorobo
Kamilisha methali.
Mwana akibebwa hutazama_____________
mbele
kando
ndivyo akuavyo
kisogo cha ninaye
Andika katika umoja.
Mihogo hiyo imeliwa na wanafunzi.
Muhogo huo umeliwa na mwanafunzi.
Mhogo huo umeliwa na mwanafunzi.
Mihogo hiyo haijaliwa na wanafunzi.
Mihogo hiyo imeliwa na mwanafunzi.
Lipi si tunda?
parachichi
ndizi
viazi
ndimu
Mtoto wa kuku huitwaje?
kikuku
jogoo
kinyaunyau
kifaranga
Andika kwa ukubwa.
Mtoto mdogo amepotea.
Toto dogo limepotea.
MTOTO MDOGO AMEPOTEA.
Watoto wadogo wamepotea.
Mtoto mdogo hajapotea.
Jaza pengo kwa usahihi.
__________ ni mwanafunzi wa gredi ya sita.
Hii
Wao
Sisi
Mimi
Jaza pengo kwa jibu mwafaka.
Ndege ametua _________ ya mti
juu ya
kando ya
chini mwa
ndani ya
Ni orodha gani iliyo na vivumishi viashiria?
hili,hicho ,kile,hayo
la kwanza,vitano,kumi, kimoja
langu, yetu,chao,wenu
nzuri,chafu,nyeusi,jipya
Tumia amba kwa usahihi.
Godoro________lililetwa ni safi.
ambalo
ambacho
ambayo
ambaye
Ukipatana na mtu aliyefiwa na mpendwa wake utamwambia_______
shikamoo
makiwa
buriani
kwaheri
Sentensi ifuatayo imetumia fani gani ya lugha?
Sifa na Sifo wanafanana mithili ya shilingi kwa ya pili.
sitiari
tashbihi
kitendawili
methali
Neno wote katika sentensi ifuatayo ni la aina gani ya maneno?
Wote wamepatikana wakiwa salama.
Kiwakilishi
kivumishi
nomino
Kielezi
Sehemu hii ya mwli huitwa________
moyo
mapafu
kibofu
mshipa
Chagua kundi lenye nomino katika ngeli ya U-I pekee.
hakimu,baharia,mtume
mpera, mkeka,gunia
pweza, mswaki,wembe
mti, miguu, mpira
Ni sentensi gani iliyo katika wakati ujao.
Huenda shuleni.
Ameenda shuleni.
Ataenda shuleni.
Haendi shuleni.
Andika kinyume cha neno "fuma"
bomoa
songa
fumua
anua
Tambua aina za maneno "mzuri" na "shuleni" katika sentensi ifuatayo.
Mtoto mzuri amekimbia hadi shuleni.
kivumishi, nomino
kivumishi, kielezi
kielezi,kiunganishi
nomino,kitenzi
