NEW
Font size
WorksheetsMASWALI
Total questions: 50
Worksheet time: 50mins
Je,nomino mkoba inapatikana katika ngeli gani?
U-U
I-ZI
U-I
U-YA
Jaza pengo.
________ tunapenda kusoma vitabu vya hadithi.
wewe
mimi
sisi
wao
Nyambua kitenzi ogopa katika kauli ya kutendesha.
ogofya
ogopwa
ogopesa
ogopeza
Ukitaka kupima kilo ya sukari utatumia nini?
utepe
rula
mizani
timazi
Ukitaka kumpima mtu nguo utatumia nini?
utepe
mizani
timazi
randa
Tumia amba kwa usahihi.
Mvua _____ hunyesha vizuri huleta manufaa.
ambayo
ambao
ambalo
ambazo
Sentensi ifuatayo iko katika wakati gani?
Sijafika mapema wala sijampata.
uliopo
timilifu
uliopita
ujao
Kanusha: Mgeni wa heshima akifika tutamkaribisha.
Mwenyeji wa heshima akirudi tutamfukuza
Mgeni wa heshima asipofika hatutamkaribisha.
Mgeni wa heshima angefika tungemkaribisha.
Mgeni wa heshima hatafika na hatutamkaribisha.
Chagua nomino ya dhahania.
maji
halaiki
kalamu
ukarimu
Ni tamathali gani ya lugha imetumika katika sentensi ifuatayo?
Akwiri ni wembe masomoni.
nahau
sitiara
tashbihi
methali
Jaza pengo.
Chumbani _________ mna uchafu mwingi.
kwao
mwao
pao
ambapo
Kamilisha methali.
Nia zikiwa moja ____________ .
kilicho juu huja
kuni huwaka
watu wanafanikiwa
kilicho mbali huja.
Shairi la mishororo mitatu katika kila ubeti huitwa_____
tarbia
tathlitha
takmisa
tathmina
Watano wamemaliza kazi ya ziada.
Neno lililopigiwa mstari ni ________
Kivumishi
kiwakilishi
kielezi
kihusishi
Kamilisha maamkizi haya.Shikamoo ni kwa marahaba kama vile waambaje ni kwa________
sina jambo
siambi
sina niambalo
sijambo au salama
Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
Mtoto mzuri amekimbia hadi shuleni.
kivumishi,nomino
kielezi,kivumishi
kivumishi, kielezi
kihusishi,kiwakilishi
Andika kwa ukubwa.
Mti huu ni mkubwa sana.
jiti hili ni kubwa sana.
Majiti haya ni ni makubwa sana.
Kijiti hiki ni kikubwa sana
Miti hii ni mikubwa sana.
Chagua sentensi sahihi.
Watu wasita walikula nyama.
Magari kumi na tatu yalinunuliwa.
Kalamu ya mwalimu ni mzuri.
Viatu vinane vimepigwa rangi.
Ni pambo lipi limeambatanishwa vilivyo?
Sikio-mapete
Mguu-kipini
Shingo-kikuba
Mkono-wanja
Ndugu na dada wa kike na wa kiume huitanaje?
umbu
mkoi
mpwa
shemeji
Tumia kiulizi kinachostahili.
Mbuzi ______waliochinjwa?
ngapi
zingapi
mangapi
wangapi
Taja neno jingine lenye maana sawa na barua.
mabarua
mtandao
anwani
waraka
Chagua sentensi iliyotumia kiwakilishi cha nafsi.
Wengine wamekamilisha kazi.
Huyu anapenda kuhifadhi mazingira.
Wangu amekamilisha kazi yake.
Sisi tunapenda kula mboga na matunda.
Wakati baina ya saa sita na saa tisa huitwa________
adhuhuri
alasiri
alfajiri
machweo
Sentensi ifuatayo inapatikana katika hali gani?
Mama angeenda sokoni angenunua matunda.
Masharti
Timilifu
mazoea
uliopita
Nomino gani zinazopatikana katika ngeli moja?
chupa, chungu, chakula
saa, dawa, meza
kioo,kitabu,kipofu
mkono,mvua,mkeka
Maneno yaliyopigiwa mstari ni mfano wa aina gani ya maneno.
Kijana aliweka vitabu ndani ya mkoba.
vihisishi
vihusishi
viwakilishi
viunganishi
Jaza pengo kwa alama ya uakifishaji ifaayo.
Mercy alienda dukani kununua___sukari, chumvi, maziwa na mkate.
;
:
'
,
Ni sentensi gani iliyoakifishwa kwa kutumia ritifaa?
Ninayajua matunda mengi:machungwa, mananasi, maembe na maparachichi.
Ng'ombe ni mnyama mwenye faida sana.
Lo! Mvua imenyesha tangu asubuhi hadi jioni.
Ukimaliza kazi umwambie mwalimu wako.
Tumeketi hapa________ saa mbili asubuhi mpaka sasa.
hadi
tangu
mpaka
asubuhi
Tutaendelea kusoma kwa bidii ______tufanye mtihani wa KPSEA.
tangu
hadi
sasa
kuanzia
Ikiwa leo ni Alhamisi,siku ya Jumapili itakuwa________
keshokutwa
mtondogoo
mtondo
juzi
Machache ni kwa mengi kama vile laini ni kwa ____
ngumu
nyembamba
ndefu
nzito
Chagua sentensi yenye nominoambata.
Clarisa aliimba wimbo mzuri.
Ukarimu unafaa katika jamii
Quiana alinunua batamzinga.
Mutie anapenda asali.
Kanusha.
Ukienda uwanjani utampata mchezaji huko.
Usipoenda uwanjani hutampata mchezaji huko.
Ungeenda uwanjani hutampata mchezaji huko.
Ungalienda uwanjani hutampata mchezaji huko.
Ukienda uwanjani hutampata mchezaji huko.
Dada yake mama nitamwitaje?
shangazi
halati
amu
binamu
Mtoto wa ndugu au dada yako anaitwaje?
mkoi
ami
mpwa
wifi
Kamilisha methali.
Achanikaye kwenye mpini ______________.
ndivyo akuavyo
sharti ainame
si mkulima
hafi njaa
Chagua jibu ambalo lina maneno ambayo si visawe.
tabasamu-nuna
rafiki-sahibu
mbogo-nyati
redio-mwengoya
Estelle alipiga miguu hadi nyumbani. Maneno yaliyopigiwa mstari ni mfano wa_______
sitiara
methali
nahau
tashbihi
Andika kinyume cha sentensi hii.
Kijana mrefu amesimama.
msichana mfupi ameketi
kijana mfupi ameketi
mzee mrefu amesimama
mzee mfupi ameketi
Pendo na Zawadi waliagana kwa kusema alamsiki. Huo ulikuwa wakati gani?
asubuhi
adhuhuri
usiku
mchana
Andika kwa wingi.
Ndizi hiyo imeiva vizuri.
Mandizi hayo yameiva vizuri.
Ndizi hayo yameiva vizuri.
Ndizi hizo zimeiva vizuri.
Mandizi hizo zimeiva vizuri.
Chagua jibu lenye maana sahihi ya nahau.
piga hatua-angalia mbele ili usuianguke.
piga hodi- subiri mlangoni ili kufunguliwa
fanya haki- kumpa mtu anachostahili kupata.
fanya bidii- endelea na shughuli fulani kwa kasi
Ni sentensi ipi iliyo katika hali ya udogo?
Kiota cha ndege kinavutia.
Kijito hicho kina maji safi.
Kiberiti kimenunuliwa na mama.
Kiwiko cha mkono wake kimepona.
Chagua jibu linalounganisha sentensi hizi kwa usahihi.
1. Trina alimpikia Serita chai.
2. Serita alimpikia Trina chai.
Trina alipikiwa chai kwa Serita.
Serita alipikia chai kwa Trina.
Trina na Serita walipikiana chai.
Serita na Trina walipikiwa chai.
Ni saa ngapi?
Saa tatu kasorobo
Saa tatu na robo
Saa tatu na nusu
Saa tatu kamili
Badala ya sabalheri, ni maamkuzi gani pia tunaweza kutumia?
Salaam aleikum
Cheichei
Chewa
Shikamoo
Chagua neno baki .
Chumvi
chuma
chakula
chandarua
Sanai alipewa shilingi elfu ishirini na wazazi wake ili aazishe biashara.Pesa alizopewa sanai huitwaje?
faida
ushuru
mtaji
riba
