wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI FORM 2

Total questions: 15

Worksheet time: 5mins

Name
Class
Date
1.

Maneno haya hufuatana vipi katika kamusi?

(i) shwari

(ii) sinzia

(iii) sentensi

(iv) staha

a)

iii, ii, i, iv

b)

ii, iii, i, iv

c)

ii, i, iii, iv

d)

iii i, ii, iv

2.

Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.

a)

Dalali alikuwa na bidhaa zifuatazo, kabati, meza, viti na rafu.

b)

Rita? hujamaliza kazi hiyo nyepesi hivyo!“

c)

Wanafunzi wake — Wale waliopata alama za juu zaidi — wametuzwa leo.

d)

Mkulima alipanda nafaka* yaani (wimbi na mtama).

3.

Wingi wa sentensi, ‘Karani yule alimpelekea mkurugenzi waraka huo’, ni:

a)

Karani yule aliwapekelea wakurugenzi waraka huo.

b)

Makarani wale waliwapelekea wakurugenzi nyaraka hizo.

c)

Makarani wale walimpelekea mkurugenzi waraka huo.

d)

Karani yule alimpelekea mkurugenzi nyaraka hizo.

4.

Chagua kauli ya kutendewa ya sentensi ifuatayo:

Menza alikwenda kwa Tumaini akakata kuni

a)

Tumaini alikatiwa kuni na Menza.

b)

Tumaini alikatiwa kuni kwa Menza.

c)

Kuni zilikatiwa Tumaini kwa Menza.

d)

Kuni zilikatiwa kwa Tumaini na Menza.

5.

Chagua jibu lenye maelezo sahihi.

a)

Kefule! ni tamko linalotumiwa kuonyesha kuudhika.

b)

Hewala! hutumiwa baada ya kuupata ushindi fulani.

c)

Simile! ni tamko linalotolewa baada ya kumruhusu mtu kupita?

d)

Makiwa! hutumiwa ili kumpa pole mtu aliyepoteza bidhaa zake.

6.

Neno lipi lenye sauti mwambatano?

a)

mvua

b)

liwa

c)

kunja

d)

wayo

7.

Kukanusha kwa, ‘Simba ambao wamejeruhiwa wametibiwa’,ni:

A.

a)

Simba ambao wamejeruhiwa hawajatibiwa.

b)

Simba ambao hawakujeruhiwa hawatatibiwa.

c)

Simba ambao wamejeruhiwa hawajatibiwa.

d)

Simba ambao hawakujeruhiwa hawajatibiwa.

8.

Chagua jibu lenye maelezo sahihi.

a)

Kufisha ni kuviweka vitu hadi viharilbike ilhali kuficha ni kuviondoa vitu mahali vinapoonekana.

b)

Kisasi ni tendo la kumlipizia mtu kosa alilotenda, na kizazi ni watu wanaoishi katika jamii moja.

c)

Zabuni ni zawadi anayopata mtu mashindanoni, na sabuni ni madini yanayotumiwa kusafisha nguo

d)

Kudanda ni kuruka ili kukishika kitu ilhali dada ni ndugu wa kike

9.

Ujanja ni kwa sungura ilhali _____ ni kwa kaburi.

a)

kawaida

b)

ghafla

c)

utulivu

d)

msiri

10.

Ni jibu lipi lisilolingana na mengine?

a)

alamsiki — binuru

b)

shikamoo ~ marahaba

c)

masalkheri — sabalkheri

d)

hodi — karibu.

11.

Chagua sentensi iliyounganisha sentensi zifuatazo ipasavyo.

Nyumba ilikuwa kubwa. Nyumba haikuwatoshea wageni wote.

a)

Mithili ya nyumba kuwa kubwa, haikuwatoshea wageni wote.

b)

Nyumba ilikuwa kubwa angalau haikuwatoshea wageni wote.

c)

Nyumba ilikuwa kubwa madhali haikuwatoshea wageni wote.

d)

Licha ya nyumba kuwa kubwa, haikuwatoshea wageni wote.

12.

Chagua sentensi inayoonyesha hali ya kuagiza.

a)

Angetaka angewaimbia.

b)

Meza tembe mbili mara moja.

c)

Watakaosoma vyema watapita mtihani wao.

d)

Uliletewa hilo.

13.

Ni sentensi ipi yenye kiambishi ‘ki’ cha ngeli pekee?

a)

Mukai alikibeba mgongoni.

b)

Shime alienda kijijini.

c)

Dola anazungumza akitabasamu.

d)

Timau akija tutafurahi

14.

Chagua jibu lenye maneno yasiyoambatanishwa ipasavyo.

a)

funguo — kicha

b)

nzige ~ wingu

c)

hindi — bunzi

d)

maji — funda

15.

Ni jibu lipi lenye vivumishi pekee?

a)

gumu, upesi, nadra, langu

b)

safi, yote, sana, halafu

c)

laini, nne, kama, mno

d)

bora, pengine, zile, kwao