Font size
WorksheetsKirejeshi amba- na -O-
Total questions: 15
Worksheet time: 1hrs 15mins
Tumia kirejeshi -o.
Gari ambalo limekwama ni la mwalimu Chapakazi.
(a)
Geuza sentensi ifuatayo iwe na kirejeshi -o:
Mtoto ambaye anaimba vizuri atatuzwa vyema
(a)
Tumia kirejeshi -o- katika sentensi ifuatayo
Shule ambayo itafunguliwa itaanza mafunzo rasmi siku ya Jumatatu.
(a)
Tumia kirejeshi -o- katika sentensi ifuatayo.
Maji ambayo yanamwagika hayazoleki.
(a)
Kiatu ambacho kinararuka ni cha kuchezea soka.
Andika upya ukitumia kirejeshi -o-
(a)
Iandike upya sentensi ifuatayo bila kutumia "amba-"
Kijiko ambacho kitatumika katika mapishi kimevunjika
(a)
Andika sentensi ifuatayo bila kutumia amba-
Nyumbani ambamo mnapikiwa wageni mmepanguswa.
(a)
Andika kwa wingi bila kirejeshi amba:
Maji ambayo yanamwagika hayazoleki.
(a)
Ni nini wingi wa:
Kipi kikusikitishacho?
(a)
Andika kwa wingi bila kirejeshi amba-:
Uyoga ambao unaliwa una sumu.
(a)
Kanusha sentensi ifuatayo:
Kikulacho kimo nguoni mwako.
(a)
Kanusha:
Simu inayokiriza ni ya Mwendawazimu Timamu
(a)
Ni nini ukanushi wa sentensi ifuatayo:
Jua linapochomoza mvua itapusa.
(a)
Andika kwa umoja:
Mayai yatakayovunjika hayatapikiwa wageni.
(a)
Sahihisha sentensi ifuatayo bila amba-
Miti ambayo inayokatwa huzuia upepo mkali.
(a)
