WorksheetsMahakamani
Total questions: 20
Worksheet time: 2hrs 40mins
Mahali ambapo kesi husikilizwa na kuamuliwa huitwa
kituo cha polisi
korti
kizimba
gereza
Anayefikiriwa kufanya kosa huitwa
mshukiwa
mshtakiwa
mlalamishi
wakili
Vikuku anavyotiwa mhalifu mkononi huitwa
ithibati
pete
vipuri
pingu
Anayepeleka kesi kortini huitwa
hakimu
shahidi
mshtaki
mshukiwa
Sehemu kama sanduku ambapo mshtaki/mshtakiwa au shahidi husimama huitwa
husuni
gereza
kizimba
jela
Mtu anayeshughulika na nyaraka za kesi kortni huitwa
jaji
karani wa korti
kiongozi wa mashtaka
mkalimani
Mahali ambapo kesi husikilizwa na kuamuliwa ni ____________
mahakama
kizimba
korokoro
jela
Mshukiwa au mhalifu anapokamatwa na polisi hupelekwa kwenye ________________
kituo cha polisi
mahakama
husuni
jela
Pesa au kitu kinachotolewa ili mshtakiwa asikilize kesi akiwa nje ya mahakama ni ______________
faini
ushahidi
ithibati
dhamana
Kamatwa na polisi ni ___________
tiwa akilini
tiwa mbaroni
funga pingu za maisha
tiwa moyoni
Pesa anazotozwa mhalifu baada ya kupatikana na kosa ni _______________
malipo
dhamana
faini
mshahara
Anayetiwa gerezani baada ya kupatikana na kosa ni (a)
Kesi kutokana na kupanga njama za kupindua serikali ni _____________
jinai
uhaini
fitina
chuki
Kitu kinachotolewa ili kuthibitisha kosa lililofanywa ni _______________
kitu kidogo
ushahidi
evidensi
vifaa
Kesi pia huitwa _______________
daawa
majukumu
hotuba
kikao
Anayeshughulikia nyaraka za kesi za mahakamani ni _______________
kiongozi wa mashtaka
jaji
karani wa korti
wakili wa serikali
Mshauri mkuu wa serikali kuhusiana na mambo ya sheria ni______________________
jaji mkuu
mkuu wa sheria
spika wa senenti
spika wa bunge la kitaifa
Anayeongoza na kuelekeza mkondo wa kesi mahakamani ni ______________
jaji mkuu
kiongozi wa kesi
kiongozi wa korti
wakili wa mshtakiwa
Anayemtetea mshtaki au mshtakiwa ni ________________
mtetezi
jaji
Mungu
wakili
Kesi iliyo na uzito mkubwa k.m. kesi ya mauaji huitwa _________________
uhaini
jinai
daawa
husuni
