Wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI DARASA LA 8

Total questions: 10

Worksheet time: 5mins

Name
Class
Date
1.

Tambua kundi lililotumia sauti ghuna pekee

a)

l, r, t

b)

e, o, u

c)

p, t, k

d)

b, d, g

2.

Tambua matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo;Wanafunzi walikula sima kwa vijiko

a)

Pamoja na

b)

Matumizi

c)

Umilikaji

d)

Uwiano

3.

Unda kivumishi cha sifa kutokana na kitenzi angalia

a)

Angavu

b)

Angivu

c)

Angalifu

d)

Angalia

4.

Teua sentensi iliyotumia kiashiria kisisitizi

a)

Simu ii hii ndiyo iliyonunuliwa

b)

Kiti hiki kizuri kitapelekwa sokoni

c)

Embe hili hili ndilo lililoliwa

d)

Mtoto mrefu alituzwa zawadi

5.

Chagua kielezi katika sentensi ifuatayo; Mtoto msikivu na mtiifu aghalabu huwatii watu wengi.

a)

Wengi

b)

Aghalabu

c)

Mtiifu

d)

Huwatii

6.

Ni jina lipi utakalolitumia kumwitia kakaye baba yako?

a)

Mpwa

b)

Mkoi

c)

Umbu

d)

Ami

7.

Ni sentensi ipi iliyotumia istiara?

a)

Juma anaweza kutamka maneno mia mja kwa sekunde

b)

Kahuthu ni duma, ana mbio sana

c)

Juma ni mrefu kama mlingoti

d)

Nilikata kiu kwa kikombe cha maji

8.

Geuza katika kauli ya taarifa : Baba aliwambia wanawe, ‘‘Viwekeni vyumba vyenu safi kila siku.’’

a)

Baba aliwahimiza wana wao waviweke vyumba vyao safi kila siku

b)

Baba alwaambia wanawe waviweke vyumba vyao safi kila siku

c)

Baba aliwaamuru wanawe kuviweka vyumba vyao safi kila siku

d)

Baba aliwashauri wanawe waviweke vyumba vyao safi kila wakati

9.

Ni sentensi ipi inayoonyesha hali ya kuagiza

a)

Mwalimu akija atawapeleka uwanjani

b)

Mulika alisikiliza ushauri akaokoka

c)

Utampata ikiwa ytazingatia mlivyoagana

d)

Msaidieni kuuinua mzigo huu

10.

Ni sentensi ipi iliyotumia kiunganishi sahihi?

a)

Sudi alipongezwa mingairi ya kupata jibu sahihi

b)

Sehemu hizi zimestawi lau kuna raia wengi

c)

Majani hayo yalipukutika laiti upepo haukuwa mkali

d)

Jengo hili ndilo imara kwa mujibu wa habari aliyotoa