wayground logo

Free Printable Worksheets

NEW

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

Sarufi :Aina Za Maneno.

Total questions: 25

Worksheet time: 19mins

Name
Class
Date
1.

Hizi ni nomino za aina gani ?(Tanzania, Nairobi, Anita, Athi, Kimbo)

a)

Kawaida

b)

Pekee

c)

Dhahania

d)

Wingi

2.

maji, maziwa, changarawe, pesa:Hizi ni nomino za aina gani?

a)

kawaida

b)

Pekee

c)

Kitenzijina

d)

Wingi

3.

Taja aina ya nomino zifuataza:


upendo, furaha, imani, elimu, ndoto, mawazo, maisha, usingizi

a)

Dhahania

b)

fungamano

c)

pekee

d)

kawaida

4.

Taja aina ya nomino zifuatazo:


kulima, kuongoza, kucheza, kulala

a)

Wingi

b)

funngamano

c)

kawaida

d)

kitenzijina

5.

Hizi ni nomino gani?: jozi la viatu, umati wa watu, bustani la maua, bunga la wanyama

a)

kawaida

b)

wingi

c)

jamii

d)

pekee

6.

Nyumba, mbuzi, daktari, soko, kalamu, jua:hii ni aina gani ya maneno?

a)

wingi

b)

Kawaida

c)

Makundi

d)

Jamii

7.

Maneno ambayo ni majina ya watu, vitu, hali huitwa?

a)

Vitenzi

b)

Nomino

c)

Vivumishi

d)

Viunganishi

8.

Maneno yanayosimamia kitendo huitwa?

a)

Nomino

b)

Vitenzi

c)

Vivumishi

d)

Viunganishi

9.

Tambua kitenzi katika sentensi ifuatayo:Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng'ambo

a)

aliwasili

b)

Mwashimba

c)

jana

d)

ng'ambo

10.

Kawia atapikia wageni.


Neno lililopigwa mstari ni---------------?

a)

kielezi

b)

kivumishi

c)

kitenzi

d)

kiunganishi

11.

Jua lilikuwa limewaka sana


Neno lililopigwa mstari ni aina gani ya kitenzi?

a)

halisi

b)

kikuu

c)

kisaidizi

d)

kishirikishi

12.

Kitenzi kisaidizi ni kipi katika senteni ifuatayo?


Bi Safina angali analala

a)

Bi

b)

angali

c)

analala

d)

Bi.Safina

13.

Kitenzi kishirikishi ni kipi?


Kaka yako ni mjanja sana.

a)

ni

b)

sana

c)

yako

d)

mjanja

14.

Neno lililopigwa mstari ni aina gani ya kitenzi Paka wake yu hapa

a)

kitenzi kikuu

b)

Kitenzi halisi

c)

Kitenzi kisaidizi

d)

Kitenzi kishirikishi

15.

Taja aina ya kitenzi kilichopigwa mstari katika sentensi ifuatayo:


Kawia atapikia wageni

a)

Kitenzi halisi

b)

Kitenzi kikuu

c)

Kitenzi kishirikishi

16.

Maneno yanayotuelezea zaidi kuhusu nomino yanaitwaje?

a)

Vielezi

b)

Vivumishi

c)

Vitenzi

d)

Vihisishi

17.

Vivumishi ambavyo hutoa sifa za kitu, mtu, mahali huitwa?

a)

Vivumishi vya pekee

b)

Vivumishi vya idadi

c)

Vivumishi vya sifa

d)

Vivumishi viulizi

18.

Tambua kivumishi:


Mvulana mkorofi aliadhibiwa na mwalimu kutokana na tabia zake mbaya.

a)

Mvulana

b)

aliadhibiwa

c)

mkorofi

d)

tabia

19.

Orodha ipi yenye vivumishi vimilikishi katika sentensi ifuatayo:


Nitatumia talanta zangu kwa manufaa ya taifa letu.

a)

Nitatumia,manufaa

b)

talanta,zangu

c)

zangu,letu

d)

taifa,ya

20.

Maneno yaliyopigwa mstari ni ?:


Aliweka kitabu chako sebuleni mwako

a)

kivumishi cha pekee

b)

Kivumishi kimilikishi

c)

Kivumishi kiulizi

d)

Kivumishi kirejeshi amba

21.

Msichana mmoja amewauwa nyoka wawili .

a)

Vivumishi vya idadi katika orodha

b)

Vivumishi vya idadi isiyokamili

c)

Vivumishi vya idadi kamili

22.

Vivumishi hivi ni vya aina gani ?


chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani

a)

isiyokamili

b)

orodha

c)

idadi kamili

23.

Jahazi lili hili

Wembe ule ule

Ng'ombe wawa hawa


Tambua kundi lenye vivumishi visisitizi pekee

a)

jahazi,wembe,ng'ombe

b)

lili hili,wawa hawa,ule ule

c)

jahazi,wawa hawa

d)

Ng'ombe ,ule ule

24.

Tambua kivumishi katika sentensi ifuatayo:


Ni walimu wangapi wamefukuzwa?

a)

Walimu

b)

Wamefukuzwa

c)

Wangapi

d)

Ni

25.

Neno lililopigwa mstari ni?


Msichana ambaye alikuja ni Sheila

a)

Kivumishi cha idadi

b)

Kivumishi kirejeshi

c)

Kkivumishi cha sifa

d)

Kivumishi kimilishi