Wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI GRADE 5

Total questions: 20

Worksheet time: 12mins

Name
Class
Date
1.

SEHEMU YA A: Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata (alama 5)

Unapotembea mjini, chukua tahadhari kubwa sana. Kuna matapeli wanaohadaa watu mjini. Vile vile matapeli hao hujiweka katika makundi ili kungojea watembezi wanaoonekana wageni. Mara wanapowagundua, wao hunasa pesa, simu na vitu vingine na kukimbia navyo. Pia kuna wale hutumia maneno matamu. Wao hukuandama na ukifika kichorochoroni watakupora na kukimbia. Wengine watakupiga na kukuacha umeumia. Iwapo unataka msaada wowote, basi mtafute bawabu au askari akusaidie. Usijiingize kwenye shida tupu bure.

Eleza maana ya neno wanaohadaa. (a)  

2.

Andika maana ya neno 'matapeli (a)  

3.

Unapofika vichochoroni huwa unafanyiwa nini? ________________________

a)

Wanakuchapa na kukimbia

b)

watakupora na kukimbia

c)

Wanakukimbiza na kukimbia

d)

Wanakupa nvitu vyako na kukimbia

4.

Kulingana na habari ni watu gani wanaoiba pesa? ___________________________

a)

matapeli

b)

wahuni

c)

walaghai

d)

waimbaji

5.

Mwandishi anatushauri tufanye nini tunapotembea mjini?

a)

Tusiongee na watu

b)

Tukimbie

c)

Tufiche pesa

d)

Tuwaulize bawabu au askari

6.

Jaza pengo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.

Waliadhibiwa ______________________ walivunja sheria za shule.

a)

Pia

b)

Kwa sababu

c)

Lakini

d)

na

7.

Jaza pengo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.

Juma alikula ______________________ hakushiba. (kwa sababu, lakini, pia)

a)

kwa sababu

b)

lakini

c)

pia

d)

ama

8.

Jaza pengo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.

Tulipita mtihani _____________ tulifanya bidii. (lakini, na, kwa sababu)

a)

pia

b)

lakini

c)

na

d)

kwa sababu

9.

Jaza pengo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.

Halima ________________ Fatuma wanaosha vyombo. (na, lakini, kwa sababu)

a)

lakini

b)

na

c)

kwa sababu

d)

ilhali

10.

Andika nomino za makundi katika sentensi zifuatazo

Barabarani kulikuwa na _______ wa magari.

a)

mlolongo

b)

safu

c)

kikosi

d)

jozi

11.

_______ ya milima hupendeza.

a)

pakacha

b)

kikosi

c)

safu

d)

mlolongo

12.

_______cha askari kilikuwa kimesimama barabarani.

a)

mlolongo

b)

safu

c)

jozi

d)

kikosi

13.

Fatuma alinunuliwa ____ ya viatu.

a)

pakacha

b)

mlolongo

c)

jozi

d)

safu

14.

Mama alinunua _____ la matunda kutoka sokoni.

a)

kikosi

b)

pakacha

c)

safu

d)

jozi

15.

Soma shairi hili kisha ujibu maswali

Nakupongeza mlezi, shuleni kunipeleka

Chakula nacho kanipa, karo pia kalipa

Mpendwa watapatapa, mimi hapa nikicheka

Pongezi mlezi wangu, kazi njema waifanya

Kanionya kaonyeka, za kulevya nikahepa,

Mbaya tabia nikaacha, masomoni, nikangara

Jukumu nilijitweka, ushauri ulionipa

Pongezi mlezi wangu, kazi njema waifanya

Shairi hili lina beti ngapi?

a)

tatu

b)

nane

c)

nne

d)

mbili

16.

Kila ubeti una mishororo mingapi?

a)

miwili

b)

mitatu

c)

minne

d)

mitano

17.

Kamilisha katika wingi.

Nguo yangu ni chafu.

a)

Nguo zangu ni chafu

b)

Manguo zangu ni chafu

c)

Manguo yangu ni chafu

d)

Nguo yangu ni chafu

18.

Kati ya nomino ulizopewa ni gani sio nomino ya dhahania?

pilipilihoho, furaha, adabu, hekima

a)

Furaha

b)

Hekima

c)

pilipilihoho

d)

Adabu

19.

Akifisha kifungu hiki.

siku moja jabali alitaka kujua zaidi kuhusu magonjwa Alimwuliza mwalimu wake maswali mengi

(a)  

20.

kitunguu, biringanya, dania, mdalasini, iliki, limau, pilipili na tangawizi ni aina ya ____________

a)

vyakula

b)

vifaa

c)

mapishi

d)

viungo