wayground logo

Free Printable Worksheets

NEW

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

MAZOEZI YA KISWAHILI

Total questions: 30

Worksheet time: 15mins

Name
Class
Date
1.

Papa ni kwa baba kama vile pipi ni kwa_________

a)

bibi

b)

popo

c)

pii

d)

biblia

2.

Maneno kama vile msichana,paka,balbu, tarakilishi,kipepeo na kizingiti kwa neno moja huitwaje?

a)

maneno

b)

vitenzi

c)

nomino

d)

vivumishi

3.

Chagua jibu lenye vitate

a)

waya,yaya

b)

nuna,tabasamu

c)

msichana, banati

d)

kiatu,soksi

4.

Mama yangu alinunua mikate__________ mitamu.

a)

nne

b)

minne

c)

vinne

d)

wanne

5.

Kamilisha sentensi kwa kivumishi kifaacho.

Dawati la mwanafunzi ni ________

a)

kipya

b)

vipya

c)

mpya

d)

jipya

6.

Cheza, imba, kimbia,ruka na soma ni mifano ya ______

a)

vitenzi

b)

vivumishi

c)

vielezi

d)

nomino

7.

Miguu ya kitanda au meza huitwaje?

a)

magurudumu

b)

matendeguu

c)

maguu

d)

vizingiti

8.

Ni maamkuzi gani yanayofaa katika picha hii?

a)

makiwa- tunayo

b)

chewa- chewa

c)

cheichei - Ewaa

d)

Shikamoo - marahaba

9.

Jibu la maagano alamsiki ni _________

a)

buriani

b)

kwaheri

c)

binuru

d)

inshallah

10.

Barua ya kirafiki ina anwani ngapi?

a)

mbili

b)

moja

c)

tatu

d)

nyingi

11.

Shairi hili ni la aina gani?

a)

tarbia

b)

tathmina

c)

takmisa

d)

tathlitha

12.

Tegua kitendawili kifuatacho.

Chalia,chatembea,na chala chakula cha mikono.

a)

b)

c)

d)

13.

Neno lililopigiwa mstari ni la aina gani?

Kijakazi anapikia chakula jikoni.

a)

kivumishi

b)

kielezi

c)

kiwakilishi

d)

kitenzi

14.

Jaza pengo.

__________ni mshororo wa shairi unaorudiwarudiwa.

a)

petu

b)

kwetu

c)

mwetu

d)

humu

15.

mashine hii huitwa kompyuta. Vilevile huitwa________

a)

dira

b)

tarakilishi

c)

chandarua

d)

runinga

16.

Kisawe cha redio ni _________

a)

mwengoya

b)

rununu

c)

tarakilishi

d)

serendani

17.

kisawe cha televisheni ni ________

a)

redio

b)

runinga

c)

bendera

d)

zulia

18.

Chagua neno baki .

a)

jokofu

b)

serendani

c)

kinu

d)

chandarua

19.

Andika kwa wingi.

Karani ameandika barua.

a)

makarani wameandika barua.

b)

karani wameandika barua.

c)

makarani yameandika barua.

d)

karani zimeandika barua.

20.

Ngeli ya A-WA hujumuisha majina ya ________

a)

wanyama pekee

b)

viumbe wenye uhai

c)

watu pekee

d)

ndege pekee

21.

Jaza pengo kwa kiambishi kifaacho.

Punda wale __mekula nyasi zote.

a)

zi

b)

wa

c)

a

d)

i

22.

Kamilisha methali.

Mtoto umleavyo ______________

a)

angali mbichi

b)

hutazama kisogo cha nina

c)

ni nyoka

d)

ndivyo akuavyo

23.

Sehemu iliyo upande mwingine wa magharibi ni_______

a)

mashariki

b)

kusini

c)

mapema

d)

kaskazini

24.

Wingi wa ubeti ni______

a)

beti

b)

mabeti

c)

mavibeti

d)

vibeti

25.

Barua pia huitwaje?____________

a)

waraka

b)

anwani

c)

dominika

d)

mtima

26.

Mstari katika shairi huitwaje?

a)

Kibwagizo

b)

Ubeti

c)

Kinu

d)

Mshororo

27.

Ndege huishi kwenye_____________

a)

Kiota

b)

Kizimba

c)

Nyumba

d)

Kasri

28.

Mimi,sisi,wewe,nyinyi,yeye na wao ni maneno ambayo huitwa___________

a)

Vivumishi

b)

Viwakilishi

c)

Vihusishi

d)

Viunganishi

29.

Kitambaa kinachowekwa kwenye dirisha huitwaje?

a)

Jokofu

b)

Rununu

c)

Pazia

d)

Kizingiti

30.

_________ ni mtungo wa kisanaa wa Kiswahili unaotungwa kwa kuzingatia sheria fulani.

a)

Kibwagizo

b)

Ubeti

c)

Shairi

d)

Tarbia