wayground logo

Free Printable Worksheets

Font size

S
M
L
XL
Worksheets

KISWAHILI 003 2021

Total questions: 15

Worksheet time: 5mins

Name
Class
Date
1.

Chagua sentensi sahihi kisarufi.

a)

Nywele ambayo imesukwa ni fupi.

b)

Ngome iliyojengwa hapa imetukinga

c)

.

Jino iliyooza imeng’olewa na daktari.

d)

Changarawe ambacho kimesombwa kitauzwa.

2.

Ukigawanya nusu mara nne sawa utapata?

a)

robo

b)

sudusi

c)

khumusi

d)

thumni

3.

Chagua jibu lenye sauti sighuna pekee.

a)

ch,f,s,th

b)

gh,j,m,t

c)

p,ny,n,d

d)

dh,k,ng’,h

4.

Nomino nyanja imo katika ngeli gani?

a)

U—Zl

b)

I—ZI

c)

I—I

d)

LI—YA

5.

Maneno yaliyopigiwa mstari na kutiwa rangi nyingine ni:

Sesi alibeba vikapu kadha begani.

a)

kielezi, kiwakilishi;

b)

kivumishi,kihusishi;

c)

kiwakilishi, kihusishi;

d)

kivumishi, kielezi.

6.

Chagua jibu la kitendawili kifuatacho. Mimi ninakula vyakula vyote vinono lakini sinenepi wala sikui.

a)

ulimi na meno;

b)

kinu cha kusagia;

c)

chungu cha kupikia;

d)

mkono na vidole.

7.

Onyesha usemi halisi wa sentensi ifuatayo. Muli aliniambia kwamba wiki ambayo ingefuata angeenda kutazama mechi hiyo.

a)

“Wiki ambayo ilifuata nilienda kutazama mechi hiyo.” Muli akaniambia.

b)

“Wiki ijayo nitaenda kutazama mechi hiyo.” Muli akaniambia.

c)

“Wiki ambayo ilipita ulienda kutazama mechi hiya.” Muli akaniambia.

d)

“Wiki ijayo utaenda kutazama mechi hiyo.” Muli akaniambia.

8.

Nukta pacha hutumiwaje?

a)

kutanguliza maneno katika orodha;

b)

kufungia maneno halisi ya msemaji;

c)

kuonyesha ufafanuzi wa maneno ya ziada;

d)

kubainisha maneno ya awali.

9.

Ni jibu lipi sahihi?

a)

Utaridi ndiyo sayari iliyo karibu sana na jua.

b)

Zebaki ndiyo sayari kubwa zaidi ya zote.

c)

Zuhura ndiyo sayari angavu yenye joto zaidi.

d)

Mshtarii ndiyo sayari iliyo karibu zaidi na dunia.

10.

Chagua sentensi iliyotumia kiunganishi sahihi.

a)

Fauka ya kumwita alikataa kuitika.

b)

Maadamu umeniomba nitakusaidia.

c)

Maria alijaribu bighairi akashinda.

d)

Umu ni msomaji bora ikiwa hanivutii.

11.

Maana ya nahau, “tia mrija” ni:

A.

B.

a)

kutumia mali vibaya;

b)

kumtegemea mtu kwa kila kitu;

c)

kujitafutia mali kwa hila;

d)

kumchukulia mtu mali ya mwenzake.

12.

Ni jibu lipi lenye maelezo sahihi?

a)

Mzegazega huuza bidhaa rejareja.

b)

Saisi hutunza wanyama wa uchukuzi.

c)

Mjume ni fundi Wa kufua visu.

d)

Sogora ni fundi wa kuimba na kukariri mashairi.

13.

Chagua kauli ya kutendewa ya sentensi hii.

Malkia alipiga ngoma akiwa kwa Hamu.

a)

Ngoma ilipigiwa kwa Hamu na malkia.

b)

Malkia alipigiwa ngoma kwa Hamu.

c)

Ngoma ilipigiwa Hamu na malkia kwake.

d)

Malkia alipigiwa ngoma na Hamu kwake.

14.

Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.

Jani hilo kavu lilipeperushwa likatua kwenye mlingoti.

a)

Majani hayo makavu yalipeperushwa yakatua kwenye mlingoti.

b)

Majani yale makavu yalipepelushwa yakatua kwenye milingoti.

c)

Majani yale makavu yalipeperushwa yakatua lovenye mlingoti.

d)

Majani hayo makavu yalipeperushwa yakatua kwenye rnilingoti.

15.

Ni jibu lipi lenye methali zenye maana sawa?

(i) Misguide uko kichwani kwapa lakutokeani jasho?

(ii) Pilipili usiyoila. yakuwashiani?

(iii) Mtama usioula wawawingiani kuku?

(iv) Kuku alaye mtama atakuwaje na nyama?

a)

(i). (iv)

b)

(ii), (iii)

c)

(i). (ii)

d)

(iii), (iv)